久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

"Kwa bahati, tumekuwa karibu sana na China" asema Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi katika mahojiano

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 03, 2023

Rais wa Tanzania Zanzibar Hussein Ali Mwinyi akihutubia kwenye ufunguzi wa Maonyesho ya tatu ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika huko Changsha, Mkoa wa Hunan, katikati mwa China, Juni 29, 2023. (Xinhua/Chen Sihan)

Rais wa Tanzania Zanzibar Hussein Ali Mwinyi akihutubia kwenye ufunguzi wa Maonyesho ya tatu ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika huko Changsha, Mkoa wa Hunan, katikati mwa China, Juni 29, 2023. (Xinhua/Chen Sihan)

CHANGSHA - Huku Dunia ikikabiliwa na changamoto kama vile mivutano ya kisiasa na mabadiliko ya tabianchi, Afrika na China zitaendelea kuwa na uhusiano wa karibu na kusaidiana, Rais wa Tanzania Zanzibar Hussein Ali Mwinyi amesema katika mahojiano na Shirika la Habari la China, Xinhua Jumamosi.

“Tumekuwa na ushirikiano mzuri tangu nyakati za kihistoria,” amesema Mwinyi ambaye amekuwa ziarani nchini China kushiriki kwenye Maonyesho ya tatu ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika yaliyofanyika hapa kuanzia Alhamisi hadi Jumapili.

Kwa miongo kadhaa, pande hizi mbili, "kama washirika wa karibu sana," zimeshuhudia "kutobadilika" katika kujitolea kwao kusaidiana, amesema Rais Mwinyi.

"Kwa bahati nzuri, tumekuwa karibu sana na China ... sera zetu zinaendana, na tutaendelea kufanya kazi na China," ameongeza.

Rais Mwinyi amesema, kuimarika kwa uchumi wa China baada ya janga la UVIKO-19 kumeleta fursa nyingi na kuingiza nguvu katika uchumi wa Afrika.

"Kwa kuona kwamba baada ya janga hili, mambo yanarudi katika nyakati za kabla ya janga (nchini China), tunafurahi kuwa hapa kuona kwamba tunafanya mambo ya maendeleo tena," amesema.

Tanzania ni nchi ya kilimo, na kupitia uwekezaji katika miundombinu na maeneo maalum ya viwanda, China inaipatia nchi ya Tanzania uwezo wa kutengeneza mazao ya kilimo na kuanzisha viwanda vya kuongeza thamani ya mazao, amesema Rais Mwinyi. "Hii ni muhimu sana kwetu."

"Nchi za Afrika zinataka kuwa na uwezo wa kujitegemea," amesisitiza Rais Mwinyi na kuongeza kuwa ushirikiano na China una umuhimu mkubwa kwao ili kufikia lengo hilo na kujenga hali yenye manufaa kwa pande zote mbili.

Akizungumzia hisia zake kwa China wakati wa ziara hiyo, Rais Mwinyi amesema kuwa "amefurahishwa sana na mafanikio yaliyopatikana nchini China: miundombinu na maendeleo, na uboreshaji wote wa uchumi."

"China inatoa mifano inayofaa kuigwa katika bara la Afrika," Mwinyi amesema. "Tunaona kuna kasi kubwa ya ukuaji wa uchumi, lakini pia tunaona mafanikio mengi katika sekta zote."

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>