Lugha Nyingine
Mshiriki?wa Maonyesho ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika kutoka Zambia aeleza matumaini ya nchi yake kuwa mshirika na China
Banda la Zambia likionekana kwenye Maonyesho ya Tatu ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika huko Changsha, Hunan, katikati mwa China (Picha na Song Ge, People's Daily Online)
CHANGSHA, Hunan - Maonyesho ya Tatu ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika yalifunguliwa Juni 29 na kufikia tamati jana Jumapili Julai 2 huko Changsha, Hunan, katikati mwa China.
Yakiwa na kaulimbiu isemayo "Kutafuta Maendeleo ya pamoja, Kunufaika na Mustakabali wa pamoja”, maonyesho hayo yamevutia kampuni na wajasiriamali waonyeshaji zaidi ya 1,000. Ukumbi wa maonyesho hayo ulikuwa umejaa watu, na waonyeshaji kutoka China na nchi za Afrika walikusanyika hapa, ambapo kuvutia wateja kwa kupitia bidhaa zao na huduma mbalimbali.
Ikiwa mojawapo ya nchi wageni rasmi katika maonyesho hayo, Zambia ilikuwa na banda linalojitegemea katika ukumbi huo ili kuonyesha rasilimali zake za utalii na utamaduni wake wa kipekee. Martha ni mwakilishi kutoka Idara ya Utalii ya Zambia. Alikaribisha kila mtu aliyekuja kwenye banda la Zambia kwa shauku: "Karibu Zambia!"
Martha amesema kuwa lengo kuu la maonyesho hayo ni kutafuta fursa za soko la utalii la China na masoko mengine, ili kufanya uhusiano kati ya China na Zambia kuwa imara zaidi. Martha ameeleza kuwa Zambia ina rasilimali nyingi za maporomoko ya maji na wanyamapori, pamoja na mandhari nyingi za asili, ambazo anatumai zinaweza kuonyeshwa kwa watalii wa China. "Kwa hivyo tafadhali chukua muda kutembelea Zambia na kuzuru nchi yetu nzuri."
Akizungumzia hisia zake kuhusu China, Martha amesema kuwa hii ni mara yake ya tatu kuja China, lakini kila mara anapokuja, anaona mambo mapya na anasisimka.
Martha amesema kuwa China ni nchi yenye uchumi mkubwa, hivyo wanatarajia kuwa mshirika wa China. Katika siku zijazo, anatumai kuendelea kwa uhusiano huu na China. "Uhusiano huo wa kiuchumi ni imara, kwa watu wa China na pia kwa watu wa Zambia.”
Martha akiwa kwenye Banda la Zambia katika Maonyesho ya Tatu ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika huko Changsha, Hunan, katikati mwa China (Picha na mwaandishi wa habari wa People's Daily Online Yuan Meng)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma