Lugha Nyingine
Uchumi wa China wadumisha mwelekeo wa kufufuka?wakati matumizi kwenye manunuzi yanapoongezeka
Picha hii ya angani iliyopigwa Juni 7, 2023 ikionyesha watalii wanaotembelea mtaa wa Taiping huko Changsha, Mkoa wa Hunan, katikati mwa China. (Xinhua/Chen Sihan) |
BEIJING - Uchumi wa China umedumisha mwelekeo wa kufufuka huku shughuli za matumizi kwenye manunuzi ya bidhaa na huduma mbalimbali zikipata nguvu na uvumbuzi zikichochewa na uboreshaji wa viwanda katika nusu ya mwaka uliopita wa 2022.
Kwenye likizo ya siku tatu ya siku ya Duanwu kuanzia Juni 22 hadi 24, China ambayo uchumi wake umechukua nafasi ya pili kwa ukubwa duniani imeshuhudia kuimarika kwa sekta yake ya utalii, ambapo jumla ya safari za watalii wa ndani milioni 106 zilifanywa na jumla yuan bilioni 37.31 (sawa na dola bilioni 5.16 za Kimarekani) zilipatikana kutokana na mapato ya utalii katika kipindi hicho. Takwimu hizo zimeongezeka kwa asilimia 32.3 na 44.5 mtawalia kuliko mwaka jana wakati kama huo, kwa mujibu wa Wizara ya Utamaduni na Utalii ya China.
Takwimu kutoka sekta ya usafiri wa anga pia zimeonyesha nia ya watu wa China kutumia fedha kwenye usafiri huo, kwani wasafiri wamefanya zaidi ya safari za anga milioni 230.65 katika miezi mitano ya kwanza, ikiwa ni ongezeko la asilimia 139.9 ikilinganishwa na mwaka jana, imesema Idara ya Usafiri wa Anga ya China.
"Tumeshuhudia ufanisi wetu wa uendeshaji na mapato ya jumla ya usafirishaji wa abiria katika nusu ya kwanza ya mwaka yakizidi kiwango cha kipindi kama hicho cha Mwaka 2019," limesema moja ya mashirika makubwa ya ndege ya China, Hainan Airlines.
Wastani wa safari za ndani za kila siku zinazoendeshwa na Shirika la Ndege la Hainan zilifikia 669 katika nusu ya kwanza ya Mwaka 2023, sawa na kiwango cha Mwaka 2019. Kwa mujibu wa shirika hilo, kiwango cha wastani cha upakiaji wa abiria kilikuwa asilimia 81.5, na njia 34 za safari za kimataifa zilianza tena kufanya kazi.
Matumizi katika bidhaa rafiki kwa mazingira na zinazotoa kaboni chache pia unakuwa mtindo maarufu kati ya watumiaji wa China, na soko la magari yanayotumia nishati mpya (NEVs) likiwa sehemu inayong'aa. Serikali za mitaa zimechukua sera kadhaa, kama vile ruzuku ya ununuzi wa NEVs na misamaha ya kodi, ili kuchochea matumizi yaliyo rafiki kwa mazingira.
Takwimu kutoka Shirikisho la Magari ya Abiria la China zinaonyesha kuwa, kuanzia Januari hadi Mei, magari ya abiria milioni 1.05 ambayo bei yake ni zaidi ya yuan 300,000 yaliuzwa kote nchini China, ikiwa ni ongezeko la asilimia 35.1 mwaka hadi mwaka. Miongoni mwao, mauzo ya NEVs yalifikia 329,770, yakiongezeka kwa asilimia 121.8 kuliko mwaka mmoja uliopita.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma