Lugha Nyingine
Kufurahia Mchezo wa Kuigiza wa “Angalia Dunhuang Tena” huko Dunhuang, China (5)
Picha ya Mchezo wa Kuigiza wa “Angalia Dunhuang Tena”. Picha kwa hisani ya wahusika wa igizo hilo. |
Ikiwa ni onesho la utumbuizaji ambalo ni la lazima kutazama kwa watu wanaofanya safari mjini Dunhuang, katika Mkoa wa Gansu wa China, Mchezo wa Kuigiza wa “Angalia Dunhuang Tena” unaonesha moyo wa uwazi, uvumilivu, ushirikiano na manufaa ya pamoja ya “Ukanda Mmoja, Njia Moja” katika mtindo wa kisanaa. Hadi tarehe 19, Juni, 2023, mchezo huo wa kuigiza umetumbuizwa mara 294, na kuoneshwa kwa watalii zaidi ya 140,000 kutoka ndani na nje ya China.
Mchezo wa “Angalia Dunhuang Tena ” uliongozwa na mwongozaji maarufu wa China Wang Chaoge. Igizo hilo kwa ujumla wake linachukua mandhari ya sehemu tano na wahusika sita kutoka historia na utamaduni wa muda mrefu wa Dunhuang. Ndani ya dakika 90 hadhira hutembea “kupita” Pango la Maandishi ya Kibuddha lenye umri wa miaka 1000 iliyopita, Pango la Mogao lenye miaka 2000 iliyopita na Njia ya Hariri yenye urefu wa zaidi ya kilomita 7,000.
“Mchanganyiko mzuri wa uimbaji na uchezaji, muziki na upangaji wa mwanga wa taa jukwaani, ni kama kusafiri kupitia zama na sehemu mbalimbali. Nimeshangazwa sana na stadi ya hali ya juu na utumizi wa hisia wa watumbuizaji,” mtalii Bi. Wu kutoka Beijing amesema baada ya kutazama igizo hilo.
“Tangu mchezo wa ‘Angalia Dunhuang Tena’ uoneshwe kwa mara ya kwanza Mwaka 2016, kwa jumla umeoneshwa mara 4,000, na kupokea watalii zaidi ya milioni 2.31 wa ndani na nje ya China. Nia yetu ya awali ya kuwekeza kwenye igizo hili ni kupitisha kwa dunia nzima ustaarabu wa China wenye maelfu ya miaka unaobebwa na Dunhuang” amesema Wang Erjiang, mzalishaji maudhui wa mchezo wa “Angalia Dunhuang Tena” ambaye pia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Utamaduni la Siku la Mkoa wa Gansu wa China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma