久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

China yazidi kuchukua hatua za kuimarisha uchumi huku ahueni ya kiuchumi ikiendelea

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 16, 2023

Picha hii iliyopigwa Aprili 27, 2023 ikionyesha mstari wa uzalishaji kwa mitambo inayojiendesha kwenye kiwanda cha Kampuni ya Zhejiang Aishida huko Wenling, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China. (Picha na Xu Weijie/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Aprili 27, 2023 ikionyesha mstari wa uzalishaji kwa mitambo inayojiendesha kwenye kiwanda cha Kampuni ya Zhejiang Aishida huko Wenling, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China. (Picha na Xu Weijie/Xinhua)

BEIJING - China imeongeza juhudi katika nyanja za sera za fedha na uwezeshaji kifedha ili kuendeleza kasi ya ukuaji wa uchumi huku takwimu mpya zikionyesha kuendelea kupata ahueni kwa uchumi, huku baadhi ya changamoto zilizobakia.

Siku ya Alhamisi, Benki kuu ya China, ilipunguza kiwango cha riba cha mwaka mmoja cha utoaji wake wa mikopo ya muda wa kati, hatua ambayo inaongeza ukwasi kwenye mfumo wa benki, kwa pointi 10 za msingi hadi asilimia 2.65. Takriban yuan bilioni 237 (dola za kimarekani bilioni 33.15) zimeingizwa sokoni kupitia mchakato huo.

Hatua hizo zinatoa ishara wazi kwamba mamlaka za serikali ya China zinafanya juhudi kubwa zaidi kuimarisha marekebisho ya kukabiliana na mzunguko wa kifedha na kufikia matarajio ya soko, wachambuzi wamesema.

Wang Qing, mchambuzi anayefanya kazi na Golden Credit Rating, amekadiria kuwa kwa kupunguzwa kwa gharama za mikopo kwa wafanyabiashara na wakaazi, mahitaji ya mkopo yatatimizwa na matumizi na uwekezaji utaimarishwa.

Uwezeshaji huo wa kifedha ulioimarishwa unakuja wakati takwimu nyingi za kiuchumi zinaonyesha kuwa uchumi wa China umeendelea katika mwelekeo wake wa kupanda, huku kukiwa na upanuzi wa sekta za viwanda na huduma, ajira imara na biashara ya nje yenye uthabiti.

Mwezi Mei, pato la viwanda nchini China lilipanda kwa asilimia 3.5 kuliko mwaka jana wakati kama huo, mauzo ya rejareja ya bidhaa za matumizi yaliongezeka kwa asilimia 12.7, na fahirisi ya sekta ya huduma ilipanda kwa asilimia 11.7, kwa mujibu wa takwimu za Idara ya Taifa ya Takwimu ya China (NBS) zilizotolewa siku ya Alhamisi. Uwekezaji kwenye mali zisizohamishika ulipanda kwa asilimia 4 katika miezi mitano ya kwanza, na kiwango cha ukosefu wa ajira mijini kilichofanyiwa utafiti kilikuwa katika kiwango cha asilimia 5.2 mwezi uliopita.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari siku ya Alhamisi, Msemaji wa NBS Fu Linghui alikiri kwamba katika mazingira magumu ya kimataifa, changamoto bado zipo, lakini pia ametaja baadhi ya maeneo yanayofanya vizuri kwa mfano ongezeko la uzalishaji, kurejea kwa matumizi na mahitaji, biashara yenye unyumbufu, ajira na bei thabiti, na maendeleo tulivu yenye ubora wa juu.

Kwenye taarifa yake mpya kuhusuuchumi wa China siku ya Jumatano, Benki ya Dunia iliendeleza makadirio yake ya ukuaji wa uchumi wa China kwa asilimia 5.6 Mwaka 2023, ikiongozwa na kuongezeka kwa mahitaji ya watumiaji. Imebainisha kuwa matumizi ya mtaji kwenye miundombinu na viwanda yanatarajiwa kubaki kuwa na unyumbufu.

Mapema wiki hii, Shirika la Nchi Zinazouza Petroli (OPEC) liliongeza makadirio yake ya kukua kwa mahitaji ya mafuta ya China Mwaka 2023 kwa mapipa 840,000 kwa siku hadi kufikia mapipa milioni 15.7, likitaja " uchumi wa China ni bora kuliko ilivyotarajiwa." OPEC hakubadilisha makadirio yake ya jumla ya mahitaji ya kimataifa ya mwaka huu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>