Lugha Nyingine
Viongozi wa Afrika watoa wito wa kuongezwa kwa juhudi za mafungamano
Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) umefunguliwa jana Alhamisi, huku viongozi wakitoa wito wa kuharakishwa kwa juhudi ili kufikia mafungamano ya kiuchumi.
Mkutano huo wa kilele uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenneth Kaunda kilichojengwa na China ulishuhudia Rais wa Zambia Hakainde Hichilema akichukua uenyekiti wa jumuiya kubwa zaidi barani Afrika kutoka kwa Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi. Mkutano huo ulifanyika chini ya kaulimbiu, "Ushirikiano wa Kiuchumi kwa COMESA Inayostawi Katika Uwekezaji wa Kijani, Ongezeko la Thamani na Utalii".
Katika hotuba yake, rais wa Zambia alisema Afrika inahitaji kuharakisha jitihada za ajenda yake ya mafungamano kwa kuondoa vikwazo ambavyo vilikuwa vinazuia muunganisho na biashara. Amesema kuna haja ya kuondoa vituo visivyo vya mipakani ili kupunguza gharama ya biashara pamoja na kuoanisha mipaka ili kufanya bara hilo kuwa na nguvu na kuimarisha biashara ya ndani. Amesisitiza kuwa mafungamano ya kikanda yatakuwa halisi endapo nchi za Afrika zitaanza kufanya maamuzi kwa ujasiri badala ya kusubiri watu wa nje.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma