Lugha Nyingine
Mashindano ya "Daraja la Lugha ya Kichina" yachochea hamu ya lugha ya Kichina nchini Ghana
Mashindano ya "Daraja la Lugha ya Kichina" nchini Ghana yamekamilika Alhamisi huku washiriki 12 wa Ghana wakiwania ubingwa. Wakati wa mashindano hayo, washiriki sio tu wameelezea hamasa na mapenzi yao kwa lugha ya Kichina kwenye hotuba zao, bali pia walifanya maonesho mbalimbali ya vipaji ili kudhihirisha ufahamu wao wa utamaduni wa Kichina ikiwa ni pamoja na kufanya mazungumzo na Opera ya Peking.
Akiongea kwenye mashindano hayo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Ghana, Wang Jimin, alisema tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2002, mashindano haya ya kila mwaka yamekuwa jukwaa muhimu kwa wanafunzi wa kimataifa kujifunza lugha ya Kichina na kuwa msukumo kwa wanafunzi kutafuta ustadi katika lugha ya Kichina. Wang amesema mashindano hayo yanaiunganisha China na sehemu mbalimbali za dunia na kutumai kuwa yatazidisha urafiki kati ya Ghana na China.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Ghana, Nana Aba Appiah Amfo, alipongeza elimu ya lugha ya Kichina nchini Ghana akisema katika Chuo Kikuu chao wanaendelea kuongeza juhudi za kuunga mkono utafiti wa Wachina kwa kuandikisha wanafunzi zaidi ya 1,000 wa shahada ya kwanza ya lugha ya Kichina.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma