Lugha Nyingine
Mashirika Manne ya Kimataifa yaongeza kadirio la ongezeko la uchumi wa China
Tarehe 7, Juni kwa saa za Paris, Shirika la Ushirikiano na Maendeleo ya Uchumi (OCED) lilitoa ripoti mpya zaidi ya kadirio la uchumi, ambayo iliongeza tena kadirio la ongezeko la uchumi wa China, na kupandisha makadirio ya ongezeko la uchumi wa China la mwaka huu na mwakani kuwa asilimia 5.4 na 5.1. OCED lilisema, kurejea kwenye hali ya kuongezeka kwa uchumi wa China kumesukuma shughuli za kiuchumi duniani.
Benki ya Dunia kwenye toleo jipya zaidi la “Makadirio ya Uchumi wa Dunia” liliyotolewa nayo tarehe 6, Juni, pia imepandisha kadirio la ongezeko la uchumi wa China la mwaka 2023 kwa asilimia 1.3.
Benki ya Dunia ilisema, mwanzoni mwa mwaka 2023, mahitaji yaliyozuiliwa katika wakati wa maambukizi ya virusi vya korona yalitolewa na kuhimiza matumizi ya ununuzi, na ongezeko la uchumi wa China lilirejeshwa kwa nguvu. Kurejea kwa uhai wa uchumi na akiba ya fedha benkini ya kupita kiasi ya hapo kabla itaunga mkono ongezeko la matumizi ya familia, hasa matumizi katika sekta ya huduma. Inakadiria ongezeko la uchumi wa China litarejea hadi asilimia 5.6.
Licha ya hayo, mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa yote yamepandisha makadirio yao ya ongezeko la uchumi wa China.
Ripoti ya katikati ya mwaka “Hali na makadirio ya Uchumi wa Dunia mwaka 2023” iliyotolewa na Umoja wa Mataifa imepandisha kadirio lake la ongezeko la uchumi wa China kuwa 5.3% kutoka 4.8% .
Ripoti mpya zaidi ya “makadirio ya Uchumi wa Asia-Pasifiki” ilikadiria kuwa, uchumi wa China unatazamiwa kuongezeka kwa asilimia 5.2 mwaka huu, na kuendelea kuwa injini ya ongezeko la uchumi wa Asia-Pasifiki hata dunia nzima.
Vitendo vya mashirika hayo ya kupandisha makadirio ya ongezeko la uchumi wa China vimeonesha maoni yao ya kuamini mustakabali wa ongezeko la uchumi wa China. Makadirio yote ya mashirika hayo manne yamezidi lengo la 5% hivi lililowekwa na China kwenye ripoti ya serikali.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma