久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

Biashara ya nje ya China yaonyesha uhimilivu kwenye ongezeko endelevu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 08, 2023

Picha hii ya angani iliyopigwa Mei 9, 2023 ikionyesha kituo cha kontena kwenye Bandari ya Lianyungang, Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China. (Picha na Geng Yuhe/Xinhua)

Picha hii ya angani iliyopigwa Mei 9, 2023 ikionyesha kituo cha kontena kwenye Bandari ya Lianyungang, Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China. (Picha na Geng Yuhe/Xinhua)

BEIJING – Thamani ya jumla ya biashara ya uagizaji na uuzaji nje bidhaa ya China iliongezeka kwa asilimia 4.7 kuliko mwaka jana wakati kama huo hadi kufikia yuan trilioni 16.77 katika miezi mitano ya kwanza ya Mwaka 2023, ikionyesha uhimilivu endelevu huku kukiwa na mahitaji duni ya nje.

Mauzo ya nje yaliongezeka kwa asilimia 8.1 kuliko mwaka jana wakati kama huo huku uagizaji bidhaa ukipanda kwa asilimia 0.5 katika miezi mitano ya kwanza, Idara Kuu ya Forodha ya China (GAC) imesema siku ya Jumatano.

Kwa vigezo vya dola ya Marekani, jumla ya thamani ya biashara ya nje ilikuwa dola za Marekani trilioni 2.44 katika kipindi hicho.

Mwezi Mei pekee, biashara ya nje iliongezeka kwa asilimia 0.5 kuliko mwaka jana wakati kama huo, ikiwa ni mwezi wa nne mfululizo wa ukuaji wa biashara ya nje, kwa mujibu wa GAC.

Takwimu zilizotolewa na GAC zinaonesha kuwa, kuanzia Januari hadi Mei, biashara kati ya China na pande washiriki wa Ushirikiano Kamili wa Kiuchumi wa Kikanda (RCEP) ilishuhudia ukuaji thabiti, unaochangia zaidi ya asilimia 30 ya jumla ya biashara ya nje ya China.

Kiwango cha ukuaji wa biashara kati ya China na Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini Mashariki (ASEAN) na Umoja wa Ulaya kilifikia asilimia 9.9 na asilimia 3.6 mtawalia.

Biashara kati ya China na nchi watia saini wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja iliongezeka kwa asilimia 13.2 kuliko mwaka jana na kufikia yuan trilioni 5.78 katika kipindi hicho.

Hasa, biashara na nchi tano za Asia ya Kati -- Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan, Turkmenistan na Uzbekistan -- iliongezeka kwa asilimia 44 , GAC imesema.

Katika kipindi cha Januari-Mei, uagizaji na uuzaji nje wa kampuni za kibinafsi uliongezeka kwa asilimia 13.1 na kufikia yuan trilioni 8.86, ikichukua asilimia 52.8 ya thamani ya jumla ya nchi nzima ya China.

Kwa upande wa aina za bidhaa, mauzo ya bidhaa za mitambo na umeme nje ya nchi yaliongezeka kwa asilimia 9.5 na kufikia asilimia 57.9 ya mauzo yote ya nje.

China imeanzisha hatua za kisera za kuleta utulivu wa kiwango na kuboresha muundo wa biashara ya nje, hali ambayo imesaidia waendeshaji biashara kukabiliana kikamilifu na changamoto zinazoletwa na kudhoofika kwa mahitaji ya nje na kuchukua ipasavyo fursa za soko, amesema Lyu Daliang, afisa wa GAC.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>