Lugha Nyingine
Kampuni ya Magari ya Ujerumani, Volkswagen yatia saini makubaliano ya uwekezaji Mashariki mwa China
Picha hii iliyopigwa Julai 4, 2022 ikionyesha karakana ya kiwanda cha Volkswagen Anhui MEB (Modular Electric Drive Matrix) inayojengwa katika Mkoa wa Anhui, Mashariki mwa China. (Xinhua) |
HEFEI - Kutokana na makubaliano ya uwekezaji yaliyotiwa saini Jumanne katika mji wa Hefei, Kampuni ya kuunda magari ya Ujerumani, Volkswagen itajenga kituo cha utafiti na maendeleo ya uundaji (R&D), uvumbuzi, na ununuzi kwa ajili ya magari yanayotumia nishati ya umeme yanaunganishwa kwenye mfumo mmoja huko Hefei, Mji Mkuu wa Mkoa wa Anhui, Mashariki mwa China.
Volkswagen imetia saini makubaliano hayo na Eneo la Maendeleo ya Kiuchumi la Hefei, ikitangaza uwekezaji wenye thamani ya takriban euro bilioni 1 (kama dola za Kimarekani bilioni 1.07) ili kuanzisha kampuni hiyo mpya mapema Mwaka 2024, ambayo inatarajiwa kuleta pamoja wataalamu 2,000 wa R&D na Ununuzi.
"Ikiwa na makao yake makuu huko Hefei, kampuni hiyo mpya yenye jina la mradi wa 100%TechCo itakuwa kituo kikubwa zaidi cha Kundi hilo la kampuni ya Volkswagen cha aina yake kuzidi mahali popote duniani. Itaunganisha magari na timu za R&D na ununuzi, huku ikiunganisha teknolojia za kisasa kutoka kwa wavumbuzi wenyeji," Amesema Ralf Brandstaetter, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Kampuni ya Volkswagen Tawi la China, katika hafla ya kusaini makubaliano.
Amesema kituo hicho kipya kinatarajiwa kupunguza hatua kwa hatua muda wa utengenezaji wa bidhaa na teknolojia mpya kwa karibu asilimia 30.
"Shukrani kwa usaidizi wa idara na maafisa wa serikali wanaohusika, tumeweza kufikia makubaliano kwa muda mfupi sana. Aina hii ya kasi ya China ni muhimu kwa kusukuma mbele mkakati wetu wa 'Ndani ya China, kwa China' kushughulikia mambo yanayoeleza mienendo ya soko katika hatua ya awali na kuharakisha hatua ya kufanya uvumbuzi," amesema Brandstaetter.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma