Lugha Nyingine
Rais Xi ampongeza Erdogan kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Uturuki
Rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za pongezi kwa Recep Tayyip Erdogan kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Uturuki.
Katika salamu zake Rais Xi amesema China na Uturuki, nchi kubwa zinazoendelea na zenye masoko yanayoibukia, zina maslahi mapana ya pamoja. Ameongeza kuwa katika miaka ya hivi karibuni, maendeleo ya uhusiano wa ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Uturuki yamedumishwa kwa kasi, na ushirikiano wa kivitendo katika nyanja mbalimbali umepiga hatua chanya.
Rais Xi amesema anathamini maendeleo ya uhusiano kati ya China na Uturuki na yuko tayari kushirikiana na Rais Erdogan ili kukuza maelewano na kusaidiana katika masuala yanayohusu maslahi ya msingi na mambo muhimu yanayofuatiliwa kwa pamoja, ili kuhimiza maendeleo endelevu, thabiti na imara ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma