Lugha Nyingine
Tanzania yaishukuru China kwa kutoa msaada wa vitabu kwa wanafunzi
Maafisa wa China na Tanzania wakihudhuria hafla ya kukabidhi vitabu vya kiada vya Lugha ya Kichina vilivyotolewa na ubalozi wa China kwa wanafunzi wa Tanzania mjini Dar es Salaam, Tanzania, Mei 25, 2023. (Picha na Herman Emmanuel/Xinhua)
DAR ES SALAAM - Serikali ya Tanzania Alhamisi ilitoa shukrani kwa ubalozi wa China nchini humo kwa msaada wa vitabu 2,700 vya Lugha ya Kichina kwa shule zinazofundisha lugha ya Kichina.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya Tanzania, Carolyne Nombo, amesema katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam, kuwa, vitabu hivyo vitasaidia kupunguza pengo la uwiano kati ya kiasi cha vitabu na idadi ya wanafunzi katika shule za sekondari na hivyo kuboresha masomo ya lugha ya Kichina.
Mwezi Aprili, ubalozi wa China pia ulitoa vitabu 2,304 vya Lugha ya Kichina kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya Tanzania na kufanya jumla ya vitabu vilivyotolewa kuwa 5,004.
“Masomo ya lugha ya Kichina yamewekwa katika shule za sekondari nchini Tanzania yameimarika sana tangu kuanzishwa kwake kama mradi wa majaribio Mwaka 2016,” amesema Nombo kabla ya kukabidhiwa vitabu hivyo na Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian.
Ofisa huyo wa Tanzania amesema, kuna shule 18 za sekondari za umma kote nchini zinazowekwa masomo ya lugha ya Kichina, na shule mbili zimeanzisha masomo ya lugha ya Kichina katika kipindi cha sekondari ya juu.
“Mipango inaendelea ya kuanzisha Chuo cha Confucius cha elimu ya msingi katika Taasisi ya Elimu Tanzania,” amesema Nombo.
Kwa upande wake Balozi Chen amesema vitabu vya kiada vilivyotolewa vitawasaidia walimu na wanafunzi wengi kujifunza zaidi historia, utamaduni na elimu ya China.
Chen amesema hadi kufikia Aprili 2023, idadi ya wanafunzi wa Tanzania wanaojifunza lugha ya Kichina katika shule 18 za sekondari za majaribio ni takriban 6,500. Kuna walimu wanne kutoka China, wanafunzi wenyeji wa Lugha ya Kichina 60, mratibu mmoja wa mradi wa China na waratibu watano wa Tanzania katika shule za msingi na sekondari.?
Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian (katikati) akimkabidhi mwanafunzi Mtanzania vitabu vya Lugha ya Kichina kwenye hafla ya kukabidhi vitabu vya kiada vya Lugha ya Kichina vilivyotolewa na ubalozi wa China mjini Dar es Salaam, Tanzania Mei 25, 2023. (Picha na Herman Emmanuel/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma