Lugha Nyingine
Kituo cha Utamaduni cha China chaandaa saluni ili kuhimiza utamaduni wa chai huko Brussels, Ubelgiji (5)
Watu wakitazama maonyesho yanayohusiana na utamaduni wa chai katika hafla ya ufunguzi wa Saluni ya Kitamaduni ya Yaji "Chai kwa Maelewano" kwenye Kituo cha Utamaduni cha China huko Brussels, Ubelgiji, Mei 4, 2023. (Xinhua/Zheng Huansong) |
BRUSSELS, - Saluni ya kitamaduni inayoangazia mbinu za kijadi za kutengeneza chai na mazoea ya kijamii ya China itafunguliwa kwa umma leo Ijumaa baada ya hafla ya ufunguzi iliyofanyika Alhamisi kwenye Kituo cha Utamaduni cha China huko Brussels, Ubelgiji.
Wageni mashuhuri waliohudhuria hafla hiyo walialikwa kuangazia utamaduni wa China kupitia sherehe za chai, uchezaji ngoma za kifahari, maonyesho na muziki.
Ikifunguliwa hadi Juni 9, shughuli hiyo inayojulikana kama Saluni ya Kitamaduni ya Yaji "Chai kwa Maelewano" itawafahamisha wahudhuriaji juu ya aina tofauti za chai kutoka mikoa 15 ya China, ikijumuisha chai ya kijani, nyeusi, nyeupe, na njano. Sherehe za chai hiyo huambatana na maonyesho ya historia ya chai ya China na mchango wake katika maisha ya watu hivi leo.
Yaji, ambayo ina maana ya "kukusanya yote ambayo ni ya kifahari" katika Lugha ya Kichina, ilikuwa njia ya kawaida kwa wasomi wa kale wa China kufurahia kwa pamoja urithi wao wa kitamaduni.
Shughuli hiyo inalenga kusherehekea kujumuishwa kwa "mbinu za kijadi za usindikaji wa chai za China na mazoea ya kijamii yanayohusiana nazo nchini China" kwenye Orodha Wakilishi ya Urithi wa Utamaduni Usioshikika wa Binadamu ya UNESCO mnamo Novemba 2022.
Pia itaadhmisha Siku ya Kimataifa ya Chai ambayo itakuwa Mei 21.
Chai ya Kichina imekuwa ikiuzwa duniani kote kwa miaka 2000, kwanza kupitia Njia ya zamani ya Hariri inayoanzia Chang'an (mji mkuu wa kale wa China) hadi Roma, Italia. Mizigo hiyo ilisafirishwa kwa muda mrefu kupitia nchi za Asia ya Kati.
"Ushirikiano wa kitamaduni na kiuchumi kati ya nchi ni msingi wa amani, kwa Ulaya na kwa Dunia nzima. Nadhani maonyesho haya yanaonyesha kwa watu wa Ulaya na duniani kote jinsi ya kuishi pamoja," Miroslav Radacovsky, Mjumbe wa Bunge la Ulaya ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwenye hafla ya ufunguzi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma