Lugha Nyingine
“Watu wanaovaa mavazi ya Hanfu” katika Mji wa Kale wa Luoyi wafuatiliwa zaidi kwenye mitandao ya kijamii (2)
Watalii wakitembelea Mji wa Kale wa Luoyi, Tarehe 12, Aprili, 2023. (Picha imepigwa na Du Mingming/People’s Daily Online) |
Hivi karibuni, watu wanaovaa mavazi ya kijadi ya China ya Hanfu wanapotembelea katika Mji wa Kale wa Luoyi huko Luoyang, China wamefuatiliwa zaidi na watu wengi kwenye mitandao ya kijamii ya China. Watu wengi zaidi wanakwenda mji huo wa Luoyi ili kujionea mvuto wa utamaduni wa kijadi wa China.
Mji wa kale wa Luoyi unaojulikana kama "feri ya katikati ya China", hivi sasa umekuwa eneo la kivutio cha utalii, na katika eneo hilo kuna majengo makongwe ya kihistoria ya China yanayohifadhiwa vizuri.
Inafahamika kuwa, ili kuwawezesha watalii kutoka sehemu mbalimbali wajue vizuri utamaduni wa “Mji Mkuu wa kale” wa Luoyang, wakati Tamasha la 40 la Kitamaduni la Maua ya Peony linapofanyika kwenye eneo la Luoyang mwaka huu, shughuli mbalimbali za kitamaduni na kitalii zitafanyika katika maeneo makuu ya vivutio vya utalii huko Luoyang.
Mandhari ya kuvutia ya Ziwa Basum katika Mkoa unaojiendesha wa Tibet, China
Katika Picha: Furahia maua ya Peony yanayochanua huko Luoyang, China
Wafugaji wa nyuki wana pilikapilika za kutafuta utajiri wakati wa maua kuchanua huko Xinjiang, China
Maua ya Pichi yachanua katika Kijiji cha Suosong, Mkoa wa Tibet, Kusini Magharibi mwa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma