Lugha Nyingine
Maonyesho ya Kimataifa ya Magari yaanza mjini Shanghai,?China (3)
Aina mpya za magari ya Yangwang yakionyeshwa kwenye Maonyesho ya 20 ya Kimataifa ya Magari ya Shanghai Aprili 18, 2023. (Xinhua/Fang Zhe) |
SHANGHAI - Maonyesho ya 20 ya Kimataifa ya Viwanda vya Magari ya Shanghai yameanza Jumanne kwenye Kituo cha Kitaifa cha Maonyesho na Mikutano (Shanghai).
Maonyesho hayo, ambayo pia yanajulikana kwa jina la Maonyesho ya Magari ya Shanghai 2023, ni maonyesho ya kwanza ya kimataifa ya magari ya daraja la A yanayofanyika nchini China tangu China kurekebisha hatua na taratibu za kukabiliana na UVIKO-19.
Zikiwa na kumbi 13 za maonyesho za ndani, maonyesho hayo yanajivunia eneo la maonyesho la mita za mraba zaidi ya 360,000.
Kwa mujibu wa waratibu wa maonyesho hayo, takriban kampuni 1,000 za magari kutoka nchi na maeneo 20 zinashiriki katika maonyesho hayo ya magari, na karibu magari 1,500 yanaonyeshwa.
Waratibu hao wanasema maonyesho hayo yataongeza imani na nguvu ya uhai katika soko la kimataifa la magari.
Kaulimbiu ya maonyesho hayo ya magari ya mwaka huu ni "Kukumbatia Zama Mpya za Viwanda vya Magari". Yamepangwa kuendelea hadi Aprili 27.
Kwa mujibu wa ratiba ya maonyesho hayo, Aprili 18 na 19 zimeteuliwa kuwa siku za vyombo vya habari, wakati Aprili 20 na 21 zimetengwa kwa wataalamu katika viwanda vya magari. Watu wataweza kutembelea maonyesho hayo kuanzia Aprili 22 hadi 27.
Mandhari ya kuvutia ya Ziwa Basum katika Mkoa unaojiendesha wa Tibet, China
Katika Picha: Furahia maua ya Peony yanayochanua huko Luoyang, China
Wafugaji wa nyuki wana pilikapilika za kutafuta utajiri wakati wa maua kuchanua huko Xinjiang, China
Maua ya Pichi yachanua katika Kijiji cha Suosong, Mkoa wa Tibet, Kusini Magharibi mwa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma