Lugha Nyingine
Maonyesho ya Tatu ya Kimataifa ya Bidhaa za Matumizi ya China yavutia kampuni?kutoka nchi wanachama wa RCEP (4)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 13, 2023
Maonyesho ya Tatu ya Kimataifa ya Bidhaa za Matumizi ya China yanayoendelea katika Mkoa wa Kusini mwa China wa Hainan yameonesha kuvutia ushiriki wa kampuni kutoka nchi wanachama wa Ushirikiano Kamili wa Kiuchumi (RCEP), kama vile, Japan, Korea Kusini, Australia na Thailand. Kampuni hizo zinatoka kwa sekta muhimu za watumiaji katika manunuzi, kama vile, manukato na arki, vipodozi, chakula na bidhaa za afya.
Kwa kushiriki maonyesho hayo, kampuni za kibiashara za nchi wanachama wa RCEP siyo tu kwamba zina fursa ya kuboresha sura ya chapa zao, bali pia kuchukua fursa ya matunda ya maonyesho hayo na sera za Mkoa wa Hainan za kutolipa kodi kuingia katika soko kubwa la wateja wa China.
(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma