Lugha Nyingine
Wafugaji wa nyuki wana pilikapilika za kutafuta utajiri wakati wa maua kuchanua huko Xinjiang, China (3)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 13, 2023
Wakati wa kuwadia kwa majira ya kuchanua na kuchavushwa kwa maua katika Tarafa inayojiendesha ya Bayingol ya Mkoa wa Xinjiang, China, siku hizi ufugaji wa nyuki umeingia kwenye kipindi cha kuzaliana kwa nyuki na uzalishaji wa bidhaa za nyuki. Hivi sasa, kuna wafuga nyuki zaidi ya 160 kwenye tarafa hiyo, na mizinga zaidi ya 60,000 ya nyuki, idadi ambayo inachukua asilimia 46 ya shughuli za ufugaji wa nyuki Kusini mwa Xinjiang.
Katika miaka ya hivi karibuni, mashamba ya ufugaji wa nyuki wa kuzaliana katika tarafa hiyo yamefanya juhudi kubwa za kutembeza aina bora za nyuki malkia na teknolojia ya kisasa ya ufugaji wa nyuki, ambapo yametembeza nyuki malkia bora zaidi ya 300, na utumiaji wao wa nyuki malkia bora umefikia zaidi ya asilimia 75.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma