Lugha Nyingine
Picha: Daraja la upinde kubwa zaidi duniani linalojengwa mkoani Guangxi, China
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 21, 2023
Picha hii iliyopigwa kutoka angani Tarehe 19, Machi ikionyesha eneo la ujenzi wa Daraja Kubwa la Tian’e Longtan katika Wilaya ya Tian'e ya Mji wa Hechi, Mkoa wa Guangxi,China. |
Daraja Kubwa la Tian'e Longtan ni mradi wa udhibiti wa barabara ya mwendo kasi kutoka Nandan hadi Tian'e Xialao. Daraja hilo lina urefu wa mita 2,488.55. Daraja kuu ni la muundo wa upinde linalojengwa kwa zege nzito, na umbali kati ya mihimili yake miwili ni wa mita 600. Litakapokamilika, litakuwa daraja kubwa zaidi kuliko Daraja la Pingnansanqiao (lenye urefu wa mita 575) na kuwa "Daraja la Upinde la kwanza duniani". Ujenzi wa daraja hilo unatarajiwa kukamilika na kuzinduliwa mwishoni mwa mwaka huu. (Picha na Chen Guanyan)
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma