Lugha Nyingine
Ushirikiano zaidi wa kifedha kati ya Marekani na China unatarajiwa na wadau wa sekta (2)
Jeffrey Ball (kushoto, kwenye skrini), msomi mkaazi katika Kituo cha Steyer-Taylor cha Sera ya Nishati na Fedha cha Chuo Kikuu cha Stanford, akitoa maelezo yake mtandaoni kwenye mjadala ulioandaliwa na Jumuiya ya Mambo ya Fedha ya Wachina nchini Marekani (ACFA) mjini New York, Marekani, Tarehe 23 Februari 2023. (Xinhua/Liu Yanan) |
NEW YORK – Wataalamu na wadao wa mambo ya fedha wamesema, Marekani na China zina uwezo wa kushirikiana katika mambo ya fedha kutokana na China kufungua mlango zaidi, ushirikiano wa pande mbili kati ya wadhibiti wa sekta na uwepo wa maslahi ya pamoja katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
Uwezo wa fursa za ushirikiano
Mingzhi Liu, profesa wa uchumi na fedha katika Chuo Kikuu cha Tsinghua PBC, chuo cha Masuala ya Mambo ya Fedha amesema China na Marekani zinaweza kukuza zaidi ushirikiano kati ya taasisi zao za mambo ya fedha, kama vile kufungua masoko ya mambo ya fedha kwa kila mmoja na katika masuala ya fedha.
“Ushirikiano kati ya Marekani na China katika mambo ya fedha unanufaisha uchumi wa nchi hizo mbili na Dunia kwa ujumla,” amesema Liu kwenye mjadala ulioandaliwa na Shirikisho la Fedha la Wachina la Marekani (ACFA) Alhamisi.
"Kwa pamoja, China na Marekani zinaweza kufanya mambo mengi," amesema Liu, akitoa mfano wa ushirikiano katika mpito wa nishati ya kijani, uwekaji fedha kidijitali na kulinda utulivu katika masoko ya mambo ya fedha.
Kufungua mlango kumeongeza mvuto
Liu amesema, kufunguliwa zaidi kwa sekta ya fedha ya China kutaleta fursa zaidi kwa wahusika wa sekta kutoka Marekani.
Liu amesema kuwa wadau wa mambo ya fedha wa Marekani wamefanya vizuri nchini China, huku wengine wakiendelea kupanua biashara zao nchini China.
Naye Bryan Lin, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huatai Securities (Marekani) amesema, China kubadili mfumo wa utoaji wa awali wa ofa kwa umma (IPO) kwa msingi wa usajili kunamaanisha kuwa vyombo vya udhibiti vya China vinaruhusu soko kuchukua jukumu kubwa zaidi katika ugunduzi wa bei ya IPO na upangaji wa bei.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma