Lugha Nyingine
China yatangaza maeneo sita ya ugunduzi wa mabaki ya kale kwa Mwaka 2022
BEIJING - Maeneo sita ya kihistoria yaliyoanzia zama za kale za vyombo vya mawe yameorodheshwa kuwa ugunduzi mpya wa mabaki ya kale wa China wa Mwaka 2022 kwenye jukwaa lililofanyika Jumatano.
Miongoni mwa maeneo hayo yaliyogunduliwa katika miji sita ya ngazi ya mkoa, mawili yanaaminika kuwa ya zama za vyombo vya mawe, na moja kutoka zama za vyombo vya shaba nyeusi.
Ugunduzi wa maeneo mawili yaliyobaki ni eneo la makaburi ya ufalme na eneo la mabaki ya kale pembezoni mwa Magofu ya Yin yaliyoanzia Enzi ya Shang (1600-1046 K.K.) na eneo la tanuri la kauri kutoka Enzi ya Xia Magharibi (1038-1227), kwa mujibu wa Taasisi Kuu ya Sayansi ya Jamii ya China, ambayo ni mratibu wa jukwaa hilo.
Eneo la zama za kale za vyombo vya mawe linalojumuisha magofu ya binadamu wa zama za kale, na wanyama na mawe yaliyochimbwa katikati mwa Mkoa wa Hubei wa China ndiyo yanaongoza orodha hiyo. Katika eneo hili, fuvu kisukuku la kichwa linaloaminika kuwa sampuli ya Homo erectus lisiloharibika zaidi ya umri wake lililopatikana katika Bara la Eurasia liligunduliwa Mwezi Desemba 2022.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma