Lugha Nyingine
Bandari ya Ganqmod iliyoko Kaskazini mwa China yarejea kazini kikamilifu (2)
Picha hii iliyopigwa Januari 25, 2023 ikionyesha malori ya mizigo yakiwa kwenye Bandari ya Ganqmod katika Mji wa Bayannur, Mkoa Unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, Kaskazini mwa China. (Xinhua/Li Yunping) |
HOHHOT - Takwimu zilizotolewa na Kamati ya Usimamizi wa Bandari zimeonesha kuwa, idadi ya jumla ya bidhaa zinazopita na kuhudumiwa kupitia Bandari ya Ganqmod, Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, Kaskazini mwa ya China ilifikia zaidi ya tani milioni 2.1 mwezi Januari, ikiwa ni ongezeko la asilimia 436.23 kuliko ile ya mwezi huo wa mwaka jana.
Idadi hiyo imeongezeka kwa asilimia 51.88 kuliko ile ya Mwezi Januari, Mwaka 2020, hali ambayo inaashiria kurejea kazini kikamilifu kwa ufanisi wa bandari hiyo baada ya China kuboresha hatua zake za kukabiliana na janga la UVIKO-19 mwishoni mwa mwaka jana.
Bandari ya Ganqmod iko katika Urad Middle Banner katika Mji wa Bayannur. Inapakana na Mkoa wa Gobi Kusini wa nchi ya Mongolia, ni bandari ya nchi kavu ya daraja la kwanza, ambayo ni njia muhimu ya kuagiza nishati, na ni bandari ya barabara yenye thamani kubwa zaidi ya biashara kwenye forodha katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani.
Bandari hiyo imeeleza kwamba, itaboresha mazingira ya biashara na kutekeleza hatua za kuwezesha biashara mwaka huu ili kufufuka kwa kasi kwa kiasi cha usafirishaji wa bidhaa.
Utaratibu wa kuingia bandarini hapo umerahisishwa, na inachukua kama sekunde 10 pekee kwa dereva wa lori wa Mongolia kuingia nchini China baada ya kukamilisha taratibu za kiforodha kama vile kujaza fomu za afya na kupita vipimo vya karantini , ili kuongeza ufanisi wa uidhinishaji kwenye forodha.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma