Lugha Nyingine
Mwanzo mzuri wa uchumi wa China wa Mwaka 2023 watarajiwa kuchochea ongezeko la uchumi wa dunia (2)
Tarehe 29, Januari, mwaka 2023, mwanamke mmoja akichukua tiketi ya filamu kutoka kwenye mashine katika semina moja ya Mji wa Guiyang wa Mkoa wa Guizhou, China. |
Viashiria na viwango vinavyotia moyo vikiwa ni pamoja na mapato ya utalii, mapato ya tiketi za filamu pamoja na faharisi ya wasimamizi wa manunuzi mwanzoni mwa Mwaka 2023 vinaunga mkono makadirio ya kuongezeka kwa kasi kuliko matarajio ya kuufufuka kwa uchumi wa China na uchumi wa dunia .
Shirika la Fedha la Kimataifa IMF Jumatatu liliinua kadirio lake la ongezeko la uchumi wa China wa mwaka 2023 kuwa asilimia 5.2 kutoka asilimia 4.4 iliyokadiriwa awali. Benki za uwekezaji, ikiwa ni pamoja na Morgan Stanley na Goldman Sachs, pia zimerekebisha makadirio yao ya ongezeko la uchumi wa China ambao ni wa ukubwa wa pili duniani.
Wanauchumi na vyombo vya habari duniani wanaona kwa kauli moja kwamba, kutokana na msingi mzuri na sera za jumla zenye ufanisi, uchumi wa China utaongezeka baada ya nchi hiyo kuboresha hatua zake za kukabiliana na maambukizi ya virusi vya korona, na utatoa msaada unaohitajika dharura kwa uchumi wa dunia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma