Lugha Nyingine
Soko la Biashara ya Kimataifa la Yiwu, China lafunguliwa baada ya mapumziko ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China (2)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 03, 2023
Alhamisi ya wiki hii, takriban wafanyabiashara 75,000 wa soko la biashara ya kimataifa ya Yiwu la Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China wamekaribisha siku yao ya kwanza ya kufanya biashara katika mwaka wa jadi wa sungura kwa kalenda ya kilimo ya China.
Katika Soko la Yiwu, kuna bidhaa za aina mbalimbali, usambazaji wa bidhaa zake ni wa kirahisi na haraka, na mazingira yake ya biashara ni mazuri, kwa hivyo linaitwa na watu kuwa “Supamaketi ya Dunia”.
Lu Rongqing, mwendeshaji wa duka la vitu vya kuchezea huko Yiwu alisema, duka lake limepata oda za bidhaa ambazo zinaweza kutolewa hadi mwezi Juni, na anakadiria thamani ya mauzo yake ya mwaka huu itaongezeka kwa asilimia 30 kuliko miaka miwili iliyopita.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma