Lugha Nyingine
Bandari ya Ningbo Zhoushan ya China yashika nafasi ya juu zaidi duniani Mwaka 2022 kwa usafirishaji wa shehena za mizigo (3)
Picha hii iliyopigwa Januari 30, 2023 ikionyesha mandhari ya bandari ya Ningbo-Zhoushan katika Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China. (Picha na Jiang Xiaodong/Xinhua) |
HANGZHOU - Bandari ya China yenye shughuli nyingi zaidi, Bandari ya Ningbo Zhoushan katika Mkoa wa Zhejiang imesema, ilishuhudia shehena yake ya mizigo ikizidi tani bilioni 1.25 Mwaka 2022, hivyo kushika nafasi ya kwanza duniani kwa mwaka wa 14 mfululizo.
Ushughulikiaji wa makontena kwenye bandari hiyo ulifikia makontena milioni 33.35 yenye urefu wa futi ishirini kila moja (TEUs) mwaka jana, na kushika nafasi ya tatu duniani.
Hadi Kufikia mwisho wa Mwaka 2022, njia za baharini za kuingia na kutoka kwenye bandari hiyo zilifikia 300, huku kukiwa na ongezeko la njia 13 kuanzia mwisho wa Mwaka 2021.
Huduma yake ya usafirishaji wa makontena kutoka kwenye njia za reli hadi baharini pia ilishuhudia ukuaji mkubwa katika Mwaka 2022, ikishughulikia makontena milioni 1.45 kwa mara ya kwanza, ikiwa ni ongezeko la asilimia 20 zaidi ya mwaka uliopita.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma