Lugha Nyingine
Vijana wa Tunisia washiriki furaha ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China (3)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 30, 2023
TUNIS – Wakishiriki mchezo wa mafumbo yenye maswali na majibu ya kushinda zawadi, kuandika Neno la Kichina "Fu", lenye maana ya Baraka, wakitengeneza Sanaa ya kukata karatasi na shughuli nyinginezo, wanafunzi wa Tunisia wamepata furaha ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China katika shughuli iliyofanyika kwenye duka la vitabu huko, Tunis, Mji Mkuu wa Tunisia siku ya Ijumaa.
Shughuli hiyo ni sehemu ya Maonyesho ya Pamoja ya Tamasha la 13 la Vitabu vya Kichina katika Maduka ya Vitabu vya Kichina Duniani, ambayo yanafanyika kwenye maduka 85 ya vitabu katika nchi na maeneo 27 duniani kote.
Wengi wa washiriki ni wanafunzi waliosoma Lugha ya Kichina kutoka Chuo cha Lugha cha Daraja la Juu katika Chuo Kikuu cha Carthage nchini Tunisia.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma