Lugha Nyingine
Shughuli za kitamaduni katika Mji wa New York, Marekani zahusisha urithi wa utamaduni usioshikika wa China (3)
Wasanii wakicheza ngoma ya kitamaduni kwenye Taasisi ya China huko Manhattan, New York, Marekani, Januari 8, 2023. (Picha na Ziyu Julian Zhu/Xinhua) |
NEW YORK - Shughuli nyingi zilionyeshwa katika Jiji la New York mwishoni mwa wiki iliyopita zikionesha urithi wa utamaduni usioshikika kutoka Suzhou, Mashariki mwa China.
Siku ya Jumamosi usiku, wasanii wa China waliwasilisha Sanaa za hariri za utarizi wa mtindo wa Suzhou, Opera ya Kunqu, na Opera ya Pingtan, ambayo ni aina ya uimbaji wa baladi katika lahaja ya Suzhou na kwa ala za Kichina, katika hafla za ufunguzi wa siku ya mandhari ya Suzhou.
Siku hiyo ya mandhari ya Suzhou ilifanyika pamoja na tamasha lililoitwa "Miangwi ya Mashairi ya Kale ya Tang " ili kusherehekea Mwaka Mpya wa jadi wa China.
"Tuna furaha sana kwamba Suzhou inafanya juhudi kubwa katika kuunganisha China na Dunia na utajiri wake wa kipekee wa kitamaduni," amesema Zhang Jun, mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa alipokuwa akihutubia kwenye hafla za ufunguzi.
Taasisi ya China, ambayo ni shirika lisilo la faida la Marekani linalojitolea kuongeza uelewa kuhusu China, Jumapili iliwakaribisha wasanii kutoka Suzhou katika shughuli za eneo la makazi ambazo karibu watu 500 walishiriki kwenye shughuli hizo.
Shen Fengying na Shen Guofang, waigizaji na waimbaji wawili mashuhuri wa Opera ya Kunqu, waliruhusu wageni kutazama sura na mwonekano wa vipodozi na mavazi yao kwa ukaribu.
Yao Huifen, gwiji mashuhuri wa utarizi wa Suzhou, amesema ameguswa moyo sana kwani washiriki wengine walilazimika kuketi sakafuni kutokana na kuwa na watu wengi kwenye shughuli zilizofanyika.
"Tunahitaji mabadilishano zaidi kama haya. Utamaduni wa jadi wa China unahitaji kwenda nje ya nchi ili marafiki wa ng'ambo waweze kuuelewa na kuuthamini," amesema Yu Junyao, mtoto wa gwiji Yao ambaye amekuwa akijishughulisha na utarizi wa Suzhou kwa zaidi ya miaka 40.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma