Lugha Nyingine
Reli mpya ya mwendo kasi yaanza kufanya kazi Kaskazini Magharibi mwa China (4)
LANZHOU - Njia mpya ya reli ya mwendo kasi yenye urefu wa kilomita 219, inayounganisha miji ya Zhongwei na Lanzhou Kaskazini-Magharibi mwa China, imeanza kufanya kazi siku ya Alhamisi.
Ikiwa imeundwa kukimbia kwa kasi ya kilomita 250 kwa saa, reli hiyo mpya inayounganisha njia ya reli ya Yinchuan-Zhongwei, imepunguza muda wa kusafiri kati ya Yinchuan na Lanzhou, miji mikuu ya Mkoa unaojiendesha wa Ningxia na Mkoa wa Gansu, hadi chini ya saa tatu.
Reli hii ya mwendo kasi pia inakamilisha sehemu ya mwisho ya njia ya reli inayounganisha mikoa ya Shaanxi, Gansu na Ningxia.
Njia hii ya reli pia inaboresha zaidi mtandao na ufikiaji wa reli ya mwendo kasi kwani inapita kwenye miji mingi mikubwa katika maeneo matatu ya ngazi ya mkoa, amesema Wang Dalin, Afisa wa Shirika la Reli la China, Tawi la Lanzhou.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma