Lugha Nyingine
Soko la utalii latarajiwa kufufuka vizuri China
Watalii wakitazama bata-mwitu katika Bustani ya Yuyuantan iliyopo Beijing, China Desemba 18. Kutokana na kutolewa kwa sera mpya za kuboresha hali ya utekelezaji wa hatua za kuzuia na kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona, vivutio vingi vya Beijing vimeanza kuwavutia watalii kama kawaida. [Picha na Feng Yongbin/Chinadaily.com.cn]
Soko la utalii la China linaweza kurudia katika hali ya kawaida katika wakati wa likizo ya Sikukuu ya Mwaka Mpya, kwani watu wanaonekana kuwa na hamu zaidi ya kusafiri katika mikoa na maeneo mbalimbali kutokana na uboreshaji wa hali ya utekelezaji wa hatua za kuzuia na kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona hivi karibuni.
Takwimu zilizotolewa na Tovuti ya utalii ya Trip.com Group zimeonesha kuwa, watumiaji karibu asilimia 60 wameoda tiketi za safari za kutembelea mikoa mbalimbali kati ya Desemba 31 na Januari 2, ikiwa ni ongezeko la asilimia 34 ikilinganishwa na lile la kipindi kama hicho mwaka uliopita. Oda za shughuli za utalii wa makundi pia zimeongezeka kwa asilimia 46 ikilinganishwa na zile za mwaka jana.
Takwimu zilizotolewa na Shirika la Utalii la Mtandaoni la Fliggy pia zinaonyesha watu wamekuwa na shauku kubwa zaidi kwa safari ndefu. Ripoti ya shirika hilo iliyotolewa siku hizi inaonyesha kuwa kuanzia Desemba 7 hadi 14, oda za tiketi za ndege za likizo ya sikukuu ya Mwaka Mpya zimeongezeka kwa mara tatu ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.
Tovuti ya utalii ya Trip.com Group imesema kuwa kutokana na kuboreshwa kwa hali ya kufuata hatua za kuzuia na kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona kwa watalii wanaoingia kwenye Mikoa ya Utawala Maalum ya Hong Kong na Macao, watalii katika mikoa hiyo wataongezeka vilevile.
Lakini, wadau wa sekta ya shughuli za utalii bado hawajawa na uhakika sana kwa ufufukaji wa soko la utalii. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Huduma za Utalii, kampuni ya ushauri wa utalii ya mtandaoni ya Ctcnn.com, Wei Changren, alisema wimbi la sasa la maambukizi ya virusi vya korona bado linaweza kuvuruga mipango ya safari wakati wa likizo, na bado itachukua muda kabla ya watu na mashirika ya utalii kurejesha imani yao.
Bwana Wei anatumai soko la utalii litakuwa na hali nzuri zaidi kabla na baada ya kipindi cha majira ya mchipuko.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma