Lugha Nyingine
Wakenya waingia kwenye msimu wa sikukuu kukiwa na kimya kutokana na kuwepo kwa shinikizo la mfumuko wa bei
Picha hii ikionyesha mandhari ya uzinduzi wa gurio la Nairobi, Kenya, Desemba 17, 2022. (Picha na Charles Onyango/Xinhua)
NAIROBI - Kwa maneno yenye ushawishi aliyofikiria kwa makini, Gideon Ray anamhimiza mteja anayetembelea duka lake la viatu vya mitumba lililoko katika mitaa yenye shughuli nyingi katikati mwa jiji la Nairobi, mji mkuu wa Kenya, kununua jozi ya viatu.
Baada ya kuhangaika kwa muda mfupi, mteja anaamua kununua jozi, jambo lililomfurahisha Ray.
Huku sherehe zikiendelea, Wakenya wanamiminika katika maduka makubwa, saloon ya urembo, na vituo vya mabasi na treni kusherehekea sherehe za Krismasi na Mwaka Mpya.
Uchunguzi wa karibu wa mitoko ya msimu wa likizo unaoheshimika, hata hivyo, unaonyesha siyo wote wanaofurahi. Ray anasema wakati wa mahojiano ya hivi majuzi kwamba ingawa watu wengi hutembelea gulio, uwezo wa kununua umepungua sana.
"Watu wanaoingia kwenye duka wanaweza kuonekana wengi lakini kati ya waingiaji ishirini, ninauza kwa watu watano tu kwa siku," amesema Ray.
Mfanyabiashara akionyesha viatu vya mitumba vinavyouzwa katika Kaunti ya Nakuru, Kenya, Septemba 1, 2022. (Picha na Sheikh Maina/Xinhua)
Ray anakiri kwamba ikiwa atashusha bei za viatu vyake zaidi, atakuwa anaanza safari ya kupata hasara, na kuongeza kuwa wateja wake wanalalamika juu ya gharama kubwa za bidhaa muhimu huku wakiwa na mapato yaliyodumaa, yaliyobanwa.
Ripoti ya hivi majuzi ya tasnia imebainisha kuwa Wakenya watakuwa wakitumia gharama ya chini kwa asilimia 17 kwenye sherehe za Krismasi kuliko walivyotumia Mwaka 2021. Wastani wa matumizi pia unatarajiwa kuwa mara 1.65 ya wastani wa mapato ya nchi hiyo, ikionesha gharama kubwa inayohusishwa na sherehe hizo.
Ripoti ya utafiti huo iliyotolewa na World Remit, imetolewa baada ya kutazama uwezo wa kumudu gharama ya chakula, na mapambo kwa wastani wa kipato cha wananchi.
Katika siku za hivi majuzi, Wakenya wameendelea kubeba mzigo mkubwa wa gharama ya juu ya chakula, nishati ya mafuta na mafuta ya kupikia. Hali hii imekuwa ikisukuma mfumuko wa bei wa kila mwezi nchini kuwa juu zaidi.
Mwezi Oktoba, mfumuko wa bei wa kila mwaka ulifikia asilimia 9.6, ikiwa ni kiwango cha juu zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu Mwaka 2017.
Vichochezi vingine muhimu vilivyotajwa kuwa chanzo cha kuleta dhiki ya kifedha ni pamoja na vita kati ya Ukraine na Russia , ambavyo vimekatiza uagizaji wa ngano na mbolea.
Zaidi ya hayo, ukame mkali wa muda mrefu unaoathiri zaidi ya kaunti 20 nchini humo unaendelea kuvamia kapu la chakula la Kenya.
Waendeshaji wa mabasi ya usafiri wa umma mjini Nairobi maarufu kama Matatu wakipakia bidhaa na vitu vya abiria wanaosafiri hadi maeneo ya vijijini kwa ajili ya sherehe za msimu wa sikukuu jijini Nairobi, Kenya, Desemba 20, 2022. (Picha na Fred Mutune/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma