Lugha Nyingine
Makampuni ya China yaenda ng’ambo kutafuta wateja ili kupata fursa za biashara na mafanikio kwenye biashara na nchi za nje
Wakati ulipokuwa na muda chini ya mwezi mmoja hadi mwisho wa Mwaka 2022 , chini ya uratibu wa serikali ya China, makampuni ya biashara ya nje ya mikoa ya Zhejiang, Jiangsu, Guangdong, Sichuan na maeneo mengi mengine yalikwenda Ulaya, Japan, Indonesia, Umoja wa Falme za Kiarabu na maeneo mengine kupanua masoko yao na kutafuta fursa za biashara.
Ikikabiliwa na hali ya kudorora kwa uchumi wa dunia na mazingira magumu ya kimataifa, shinikizo la uzalishaji na uendeshaji wa makampuni ya biashara ya nje imeongezeka zaidi. Wataalamu wa sekta ya biashara ya nje wanaona kwamba maeneo mengi yameratibu makampuni ya biashara kwenda nje ya nchi "kukamata oda" na "kuvutia uwekezaji", ambayo inaonyesha kuwa makampuni ya biashara ya China yanafanya juhudi kubwa ili kujipatia maendeleo , na kuongeza zaidi imani ya kudumisha ongezeko tulivu.
Waendeshaji wengi wa makampuni ya biashara ya nje walisema kuwa baada ya kutokea kwa janga la Virusi vya Korona, mawasiliano na wateja wa nje yamekuwa magumu, mahusiano yamevurugika na oda zimepungua. Kutokana na uboreshaji wa taratibu na hatua za kuzuia na kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona nchini China, serikali imefanya juhudi za kuhamaisha makundi ya uchumi na biashara kwenda nje "kukamata oda", jambo ambalo linawafanya waone matumaini na kujaa nguvu.
Li Dawei, mkurugenzi na mtafiti wa Ofisi ya Utafiti wa makundi ya Uchumi yanayojitokeza ya Idara ya Utafiti wa Uchumi wa Kigeni katika Taasisi ya Utafiti wa Uchumi ya China, anasema, "kuwawezesha wahitaji oda zaidi wa ng'ambo kuwa na mawasiliano ya ana kwa ana na makampuni mbalimbali ya China , na kupunguza gharama za biashara ni muhumu sana kwa kuhimiza maendeleo ya sifa bora ya biashara ya nje ya China ."
Tokea mwaka huu, hatua mbalimbali zimetolewa na Serikali Kuu na mikoa ili kusaidia kuvunja "kizuizi" cha maendeleo ya biashara ya nje, kuunga mkono bidhaa bora kufungua na kupanua masoko ya kimataifa, na kusaidia makampuni kushiriki kwenye maonesho mbalimbali ili kujipatia oda .
Takwimu zilizotolewa na Idara ya Forodha ya China zimeonesha kuwa, katika robo tatu za kwanza za mwaka huu, thamani ya jumla ya uagizaji na uuzaji wa bidhaa ya China ilikuwa Yuani trilioni 31.11, ikiwa ni ongezeko la 9.9% ikilinganishwa na lile la kipindi kama hicho mwaka uliopita. Sera na hatua za kusaidia makampuni kutatua matatizo na kulinda makampuni zimetekelezwa kwa hatua madhubuti, na ongezeko la biashara ya nje ya China imepata mafanikio dhahiri.
"Mahitaji ya ng’ambo juu ya viwanda vya utengenezaji bidhaa vya China ni makubwa, na ongezeko la mauzo ya bidhaa za teknolojia ya juu vimekuwa hali mpya ya maendeleo yenye sifa bora ya biashara ya nje." Pan Helin, mkurugenzi na mtafiti katika Kituo cha Utafiti wa Uchumi wa Kidijitali na Uvumbuzi wa mambo ya Fedha katika Chuo cha Biashara ya Kimataifa cha Chuo Kikuu cha Zhejiang, amesema, kiwango cha sasa cha mfumuko wa bei duniani ni cha juu, bidhaa za teknolojia ya hali ya juu ya China zina bei nafuu, soko lake la mauzo ya nchi za nje litapanuliwa zaidi.
Thamani ya biashara ya nje imezidi dola za kimarekani trilioni 6; ambayo China imedumisha nafasi yake ya nchi inayoongozazaidi duniani katika biashara ya bidhaa duniani kwa miaka mitano mfululizo... Katika miaka mingi iliyopita, biashara ya nje ya China imeendelea kupata nguvu yake na kurekebisha muundo wake na kuongeza ubora na nyongeza za thamani hatua kwa hatua, na "Bidhaa zinazotengenezwa na China" zimekaribishwa na nchi nyingi.
"Hivi sasa, kutokana na kuongezeka kwa gharama za uzalishaji bidhaa kama vile nguvu kazi na ardhi nchini China, shinikizo la ushindani linaloyakabili makampuni ya biashara ya nje yanayotumia nguvu kazi kubwa kama vile viwanda vya nguo limeongezeka." Li Dawei anasema kuwa China inapaswa kutegemea bidhaa zenye sifa bora na kuendelea kuongeza uwezo wa uzalishaji wa bidhaa unaohitaji nguvu kazi kubwa, kuchukua nafasi ya hali ya juu katika minyororo ya uzalishaji wa bidhaa husika, ili kujipatia nyongeza zaidi ya thamani ya bidhaa na kuongeza nguvu ya ushindani wa kimataifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma