Lugha Nyingine
Uchumi wa Kenya wakadiriwa kukua kwa asilimia 5.8 kwa mwaka huu
(CRI Online) Desemba 22, 2022
Uchumi wa Kenya unatarajiwa kukua kwa asilimia 5.8 kwa mwaka huu, ikiwa ni kukua kwa kupungua kutoka asilimia 7.5 ya Mwaka 2021.
Ripoti iliyotolewa na Taasisi ya Kenya ya Utafiti na Uchambuzi wa Sera ya Umma (KIPPRA) inasema ukuaji huo utasaidiwa na kurejea kwa shughuli za ununuzi wa bidhaa na matarajio ya kufufuka kwa sekta zote za uchumi.
Sekta ya kilimo inakadiriwa kukua kwa asilimia 2.3 ikilinganishwa na kupungua kwa asilimia 0.2 kulikorekodiwa Mwaka 2021 kutokana na ukame unaoshuhudiwa nchini Kenya.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma