Lugha Nyingine
China yafanya Mkutano wa Kamati Kuu ya Kazi ya Uchumi kupanga mpango wa Mwaka 2023
Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, Rais wa China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China, akitoa hotuba muhimu kwenye Mkutano wa mwaka wa Kamati Kuu ya Kazi ya Kiuchumi uliofanyika Beijing China kuanzia Desemba 15 hadi 16. (Xinhua/Ju Peng)
Mkutano wa mwaka wa Kamati Kuu ya kushughulikia mambo ya Uchumi umefanyika Beijing mwishoni mwa wiki kuanzia Alhamisi hadi Ijumaa kwa ajili ya viongozi wa China kupanga na kuamua vipaumbele vya kazi ya uchumi kwa Mwaka 2023.
Akitoa hotuba muhimu kwenye mkutano huo, Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, Rais wa China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China, alifanya majumuisho kuhusu kazi za China za uchumi kwa Mwaka 2022, kuchambua hali halisi iliyopo ya kiuchumi na kupanga kazi ya uchumi ya mwaka ujao.
Li Keqiang, Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Han Zheng, Cai Qi, Ding Xuexiang and Li Xi walihudhuria mkutano huo.
Ilielezwa kwenye mkutano huo kwamba kwa ujumla kufufuka na kuimarika kwa uchumi wa China kunatarajiwa kwenye ufanisi wa uchumi katika mwaka ujao na kwamba imani ya kithabiti ni muhimu kwa ajili ya kufanya kazi nzuri kwenye kazi ya uchumi.
Mkutano huo umeagiza kuleta uthabiti wa uchumi kuwa kipaumbele cha juu na kupiga hatua nzuri huku uthabiti wa uchumi ukihakikishwa katika mwaka ujao.
Sera tendaji ya kibajeti na sera makini ya kifedha itaendelea kutekelezwa mwaka ujao. Wakati huo huo, juhudi zitafanywa kuimarisha udhibiti wa uchumi mkuu na kuratibu sera mbalimbali ili kuunda harambee kwa ajili ya maendeleo ya kiwango cha juu, kwa mujibu wa mkutano huo.
Mkutano huo umesisitiza kuwa sera za viwanda zinapaswa kuboreshwa ili kuwezesha mageuzi na uboreshaji wa viwanda vya jadi na kuratibu na kukuza viwanda vinavyojitokeza kimkakati, pamoja na kuimarisha muunganisho dhaifu katika minyororo ya viwanda, na kuviwezesha viwanda viwe na nguvu mpya za ushindani katika lengo la China la kufikia kilele na kutokuwepo kwa kaboni.
Kwa upande wa sera za sayansi na teknolojia, China itatekeleza miradi muhimu ya sayansi na teknolojia katika ngazi ya kitaifa, ikitoa mchango kamili kwa jukumu la serikali katika kuongoza kazi ya kuleta mafanikio katika teknolojia muhimu na za msingi na kuangazia jukumu kuu la makampuni ya biashara katika uvumbuzi wa kiteknolojia, umesema mkutano huo.
Mkutano huo pia umesema, sera za kijamii zinapaswa kuhakikisha maisha ya watu, kuweka kukuza ajira kwa vijana, hasa wahitimu wa vyuo vikuu, katika kipaumbele cha juu, na kujitahidi kupunguza athari za kupanda kwa bei za miundo kwa baadhi ya wale walio katika matatizo kwa wakati na kwa ufanisi.
Huku ukifafanua kuwa kuna wingi wa majukumu katika kazi ya kiuchumi Mwaka 2023, mkutano huo umesisitiza hatua za kuboresha matarajio ya umma na kuongeza imani kwa maendeleo.
Mkutano huo umehimiza juhudi za kuimarisha mageuzi ya viwadna vya kiserikali sambamba na kuboresha ushindani wao wa kimsingi, unaohitaji kwamba mipango ya kisheria na kitaasisi lazima ifanywe ili kuhakikisha usawa wa mashirika ya kibinafsi na viwanda vya kiserikali.
Mkutano huo pia umesisitiza kuzuia kwa ufanisi na kupunguza hatari kubwa za kiuchumi na kifedha, kuhimiza maendeleo thabiti ya soko la mali, kuhakikisha ukamilishaji na uwasilishaji wa nyumba zilizouzwa hapo awali na kukidhi mahitaji ya kifedha ya sekta hiyo.
Waziri Mkuu wa China Li Keqiang akihutubia kwenye mkutano wa mwaka wa Kamati Kuu ya Kazi ya Uchumi hapa Beijing, China. (Xinhua/Ju Peng)
Li Qiang, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) akizungumza kwenye Mkutano wa Mwaka wa Kamati Kuu ya kazi ya uchumi uliofanyika Beijing, China. Mkutano. (Xinhua/Yan Yan)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma