Lugha Nyingine
Wachina waliorejea kutoka ng’ambo na Wanakijiji wanaungana kustawisha kijiji nchini China
Hefei - Katika muda wake wa ziada, Guo Shanqiuyun anapenda kuzunguka-zunguka katika kijiji cha milimani, akiwa amembeba mtoto wake mchanga mikononi mwake, akipiga soga na wanakijiji njiani, na kufurahia mguso wa kibinadamu kijijini.
Guo na mumewe, ambao wote walisoma nje ya nchi na kufanya kazi katika Mji wa Shenzhen ulioko Kusini mwa China, walichagua kuishi katika Kijiji cha Tangjiazhuang katika Mji wa Huangshan, Mkoa wa Anhui, Mashariki mwa China, baada ya miaka mingi ya maisha ya kusukumwa katika miji mikubwa.
Kijiji hicho kilicholala kinaweza kisionekane cha kipekee kikilinganishwa na vijiji vingi vya kale vya Anhui vilivyo na historia ndefu na tamaduni za kina. Hata hivyo, kwa wanandoa hao, kurudisha kijiji kama hicho katika maisha na nguvu yake ni jambo gumu lakini la kupendeza linalostahili kujitoa kwa mtu.
"Badala ya kuendesha biashara ya loji, tunataka kuchangia maendeleo ya kijiji," anasema Zhang Li, mume wa Guo, ambaye pia ni msanifu wa ramani ya ujenzi ambaye alichoshwa na uchache wa mandhari ya kisasa ya mijini. Mandhari ya kipekee ya kijijini Tangjiazhuang inaonekana kumvutia zaidi.
Mwaka 2015, Guo na Zhang, wakiwa na utaalam katika masoko na usanifu mtawalia, waliwekeza na kujenga eneo la mapumziko la utalii la vijijini ambalo linajumuisha huduma ya malazi, eneo la kambi, mgahawa na baa, na kadhalika.
"Ustawishaji wa vijiji hauwezi kupatikana kwa kuwekeza pesa tu. Falsafa yetu ni kwamba tunapaswa kuweka watu mbele na kupata manufaa katika ushirikiano na wanakijiji," Guo amesema.
Wazo lao linaendana na mpango wa kijiji. "Ingawa kijiji chetu kimejaliwa kuwa na mandhari nzuri, hakishuhudia watalii wengi wanaokuja kwa sababu ya eneo lake la mbali," anasema Jiao Guibao, Katibu wa Chama wa kijiji hicho, na kuongeza kuwa karibu vijana wote walikuwa na tabia ya kuondoka kijijini kufuata ndoto katika miji mikubwa, na kuacha wazee nyuma.
"Tumeungana ili kujenga Tangjiazhuang kuwa jamii yenye furaha katika maeneo ya vijijini ya China. Guo na mumewe wametuletea tasnia kadhaa na vipaji, na kuwavutia vijana kurudi katika kijiji chao," Jiao ameongeza.
Li Weifu, ambaye ni fundi wa mianzi mwenye umri wa miaka 70, anatoa ushuhudia wa kunufaika na mabadiliko katika kijiji hicho katika miaka ya hivi karibuni. Alikuwa akiuza bidhaa zake za mianzi kwenye masoko ya ndani. Sasa, ukumbi wa maonyesho wa bidhaa zinazotokana na mianzi umeanzishwa katika kijiji ili kuonyesha kazi zake za mikono.
"Watalii wengi wanavutiwa na ujuzi wangu wa kusuka na kununua bidhaa za mianzi kama vile mapambo ya nyumbani," Li amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma