Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping afanya mazungumzo na Rais wa Mongolia
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amefanya mazungumzo na Rais wa Mongolia Ukhnaagiin Khurelsukh Jumatatu kwenye Jumba Kuu la Mikutano ya Umma la Beijing wakati wa ziara yake nchini China.
Xi amemkaribisha Khurelsukh na kusema kwamba marais hao wawili kukutana tena baada ya miezi miwili kama walivyoahidi kunaonyesha kikamilifu kiwango cha juu cha uhusiano kati ya China na Mongolia.
Xi amesema nchi hizo mbili ni jirani muhimu wa kila mmoja. Ni kwa masilahi ya kimsingi ya watu wa pande mbili kudumisha uhusiano wa muda mrefu na thabiti wa ujirani mwema, urafiki na ushirikiano. Amesema, kwa kufuata kanuni ya upendo, unyoofu, kunufaishana na ujumuishaji wa watu wote, China inaendeleza urafiki na ushirikiano na nchi jirani. Inaona umuhimu mkubwa katika kukuza urafiki, kuaminiana na maslahi ya pamoja na Mongolia.
Xi amesema, nchi hizo mbili zimesaidiana katika kupambana na UVIKO-19, na kuimarisha urafiki wa jadi katika safari. Mazungumzo na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika nyanja mbalimbali yamepata maendeleo madhubuti, na kutoa mfano mzuri wa uhusiano kati ya nchi na nchi, Xi amesema.
Rais wa China ameelezea kuhusu Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na vipengele vitano vya maendeleo ya kisasa ya China. Amesema wakati CPC inaongoza watu wa makabila yote ya China kuelekea ustawi wa taifa katika nyanja zote kupitia njia ya maendeleo ya kisasa, China haitatambua tu ustawi wake lakini pia itachangia ujirani wake na zaidi kupitia maendeleo yake.
Huku akisisitiza kuwa China na Mongolia zitaheshimu uhuru, mamlaka, ukamilifu wa ardhi na chaguo la njia ya maendeleo wa upande mwingine, Xi amesema pande hizo mbili zitatafuta maelewano zaidi kati ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, Pendekezo la Maendeleo ya Dunia na Sera Mpya ya Ufufuaji Uchumi ya Mongolia.
Xi amesema China iko tayari kuongeza ushirikiano na Mongolia katika nyanja muhimu za uchumi, biashara, nishati, madini na uunganishaji, huku ikipanua ushirikiano katika teknolojia ya habari na usindikaji wa kina wa mazao ya mifugo.
Kwa upande wake Khurelsukh ametoa pongezi kwa mara nyingine tena kwa kufanikiwa kwa Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC na kumpongeza Rais Xi kwa kuchaguliwa tena kuwa Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC.
Amesema, upande wa Mongolia una furaha kuona kwamba chini ya uongozi wa CPC, China imefanikiwa kutimiza lengo lake la kwanza la miaka mia moja. Amesema, Mongolia inaamini kwa dhati kwamba Katibu Mkuu Xi na CPC wataendelea kuwaongoza watu wa China katika kuijenga China kuwa nchi kubwa ya kijamaa yenye maendeleo ya kisasa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma