Lugha Nyingine
China yazindua jukwaa la kwanza la huduma za kiufundi za biashara kwa Afrika
(CRI Online) Novemba 10, 2022
Kituo cha Utafiti na Tathmini kuhusu Mbinu za Kiufundi za Biashara cha China na Afrika kimezinduliwa mjini Changsha, Mkoa wa Hunan nchini China na kuwa jukwaa la kwanza la huduma za kiufundi za biashara la China kwa Afrika.
Hafla ya kuanzishwa kwa kituo hicho imefanyika kwenye Maonyesho ya Tano ya Kimataifa ya Uagizaji wa Bidhaa ya China (CIIE) yanayoendelea mjini Shanghai.
Kazi za kituo hicho ni pamoja na kukusanya taarifa, kutoa huduma za ushauri, kufanya uchunguzi wa athari, na kuhimiza usawazishaji wa vigezo. Kutokana na msaada wa jukwaa la kidijitali, kituo hicho kitakukusanya taarifa za mbinu za kiufundi za biashara za nchi 54 za Afrika, ili kutoa msaada wa kiufundi na huduma za kubadilishana taarifa za kiufundi kuhusu biashara.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma