Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping akutana na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 24, 2022
BEIJING - Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Jumapili alikutana na zaidi ya wajumbe 2,700, hususani wajumbe waalikwa maalumu na washiriki wasiopiga kura wa Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC mjini Beijing, China.
Xi, ambaye pia ni Rais wa China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China, alipokelewa kwa shangwe na nderemo nyingi kwenye Jumba Kuu la Mikutano ya Umma ya Beijing. Alipata wasaa wa kupiga picha pamoja na wajumbe hao.
Viongozi wengine pia walishiriki katika mkutano huo.
Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC ulifanyika kuanzia Tarehe 16 hadi 22 Oktoba mjini Beijing.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma