Lugha Nyingine
CPC chatangaza viongozi wa juu wapya kwa safari ya kuelekea maendeleo ya kisasa ya China (2)
Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na wajumbe wengine wapya waliochaguliwa wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya 20 ya CPC Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang na Li Xi, wakikutana na waandishi wa habari kwenye Jumba Kuu la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Oktoba 23, 2022. (Xinhua/Shen Hong) |
BEIJING - Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Jumapili kimetangaza uongozi wake mpya wa juu, ambao utaongoza nchi hiyo yenye watu wengi zaidi duniani katika safari yake mpya kuelekea nchi kubwa ya kijamaa yenye maendeleo ya kisasa katika sekta zote.
Xi Jinping amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China kwenye kikao cha kwanza cha Kamati Kuu ya 20 ya CPC kufuatia mkutano mkuu wa 20 wa CPC uliofanyika katika muongo mmoja kukamilika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Akipokelewa kwa shangwe na nderemo nyingi, Xi aliwaongoza Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang na Li Xi kwenye jukwaa la zulia jekundu kwenye Jumba Kuu la Mikutano ya Umma la Beijing.
Hawa ni wajumbe wa Kamati ya Kudumu iliyochaguliwa hivi karibuni ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC.
Kwa mujibu wa Katiba ya CPC, vyombo vya juu vya uongozi vya Chama ni Mkutano Mkuu na Kamati Kuu ambayo mkutano huo huichagua. Kupitia vikao vya Kamati Kuu, Ofisi ya Siasa na Kamati yake ya Kudumu itatekeleza majukumu na mamlaka ya Kamati Kuu.
Kamati Kuu ya 20 ya CPC ilichaguliwa Jumamosi katika kikao cha kufunga Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC.
Akizungumza na waandishi wa habari zaidi ya 600 kutoka ndani na nje ya nchi, Xi amepongeza mkutano huo akiuelezea kuwa umeshikilia bendera yake juu, umeunganisha nguvu zote, na kuhimiza mshikamano na kujitolea.
Xi ameeleza shukrani kwa imani ambayo Chama kizima kimeweka kwa uongozi mpya mkuu.
"Tutazingatia asili na madhumuni ya Chama na dhamira na wajibu wetu wenyewe, na kufanya kazi kwa bidii katika kutekeleza wajibu wetu, ili kuthibitisha kuwa tunastahili uaminifu mkubwa wa Chama na watu wetu," amesema.
Ameeleza kuwa, China ikiwa imekamilisha ujenzi wake wa jamii yenye maisha bora kwa pande zote , sasa inapiga hatua kwa kujiamini katika safari mpya ya kuijenga China kuwa nchi ya kijamaa yenye mambo ya kisasa katika mambo yote.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma