Lugha Nyingine
Mtaalamu asema makampuni ya China yatoa mchango mkubwa katika uchumi wa Kenya
Gari likiendeshwa kwenye Barabara Kuu ya Nairobi nchini Kenya, Julai 31, 2022. (Xinhua/Long Lei)
NAIROBI - Makampuni ya China yanatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Kenya, mtaalam wa uchumi amesema Jumanne wiki hii.
Judd Murigi, Mkuu wa Utafiti wa kampuni ya usimamizi wa uwekezaji ya ICEA LION Asset amesema mjini Nairobi, Kenya, kwamba makampuni ya China yamekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya barabara, reli, nyumba za bei nafuu pamoja na miradi mingine mingi ya miundombinu.
Murigi ameeleza kuwa makampuni ya China pia yameanzisha maeneo ya viwanda vya kutengeneza bidhaa kwa ajili ya wateja ambavyo vimeajiri wenyeji na pia kupunguza gharama za uagizaji wa bidhaa.
"Hii ni hatua nzuri kwa sababu ni viwanda ambavyo vinaendesha mageuzi ya kiuchumi," amesema kwenye uzinduzi wa ripoti ya uwekezaji ya robo ya nne ya Mwaka 2022.
Amebainisha kuwa China ikiwa soko linaloibukia inaweza kutambua fursa za kipekee za uwekezaji nchini Kenya ambayo ni soko la bidhaa la kimataifa.
Murigi amesema kuwa makampuni ya China yamepata mafanikio nchini Kenya kwa sababu yanabadilika na kuthamini changamoto na fursa zilizopo nchini Kenya, na kupendekeza kuwa Kenya inaweza kujifunza kutoka kwa China kwa sababu imeonyesha jinsi inavyoleta mabadiliko chanya kwenye uchumi katika kipindi kifupi.
Picha iliyopigwa Mei 8, 2022 ikionyesha sehemu ya Barabara Kuu ya Nairobi, Kenya. (Xinhua/Dong Jianghui)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma