Lugha Nyingine
Mchakato wa "Maendeleo ya Mambo ya Kisasa ya China” waandikwa katika ripoti ya mkutano mkuu wa CPC
BEIJING – Mchakato wa maendeleo ya mambo ya kisasa ya China, ambao ni eneo muhimu linalofafanua safari ya China ya ustawishaji mpya wa taifa, kwa mara ya kwanza umeandikwa katika ripoti ya Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), chama kikubwa cha Ki-Umarxi kinachoongoza duniani.
Katika ripoti yake ya Jumapili kwenye Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China, Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC, alisisitiza "kazi kuu" ya Chama, akitaka juhudi za ustawishaji wa Taifa la China katika sekta zote "kupitia njia ya China ya maendeleo ya mambo ya kisasa."
Picha hii iliyopigwa kutokea angani ikionyesha mwonekano wa Bandari ya Kimataifa ya Kontena ya Yangpu katika Eneo la Maendeleo ya Kiuchumi la Yangpu, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, Mei 26, 2021. (Xinhua/Pu Xiaoxu)
Maono yaliyo wazi na yenye malengo
Wakati wavamizi wa Japani walipoitumbukiza China katika hatari miaka ya 1930, mwanahistoria mashuhuri wa China alitafakari na kuibua swali ambalo lilikuwa likimsumbua kwa muda mrefu yeye na wenzake: Je, Wachina wanaweza kufanya maendeleo ya mambo ya kisasa?
Leo jibu la swali hilo linaonekana kwa kila mtu. China ambayo ina uchumi wa pili kwa ukubwa duniani imepata mafanikio ndani ya miongo kadhaa iliyopita, ambayo yalizichukua karne kadhaa nchi za Magharibi kuyafikia.
China imeondoa umaskini uliokithiri na kumaliza kujenga jamii yenye ustawi katika sekta zote, hivyo kukamilisha lengo la miaka 100 ya kwanza tangu kuanzishwa kwa CPC.
Kwa mujibu wa mpango mkakati wake wa hatua mbili, CPC itaiongoza China kwenye hatua inayofuata katika kuelekea "nchi ya kijamaa yenye mambo ya kisasa kuanzia Mwaka 2020 hadi 2035," na "kuijenga China kuwa nchi ya kijamaa ya kisasa yenye ustawi, nguvu, demokrasia, maendeleo ya kitamaduni, yenye usawa na ya kuvutia kutoka Mwaka 2035 hadi katikati ya karne hii."
Picha hii inaonyesha mandhari ya usiku ya barabara ya kibiashara katika Mji wa Wuhan, Mkoa wa Hubei katikati mwa China, Tarehe 2 Julai 2022. (Xinhua/Xiao Yijiu)
Safari ya kipekee
Mchakato wa maendeleo ya mambo ya kisasa ya China una vipengele ambavyo ni vya kawaida kwa michakato ya ujenzi wa mambo ya kisasa ya nchi zote, lakini unajulikana zaidi na vipengele ambavyo ni vya kipekee kwa umaalum wa China.
Xi alisema maendeleo ya mambo ya kisasa ya China ni mambo ya kisasa yenye idadi kubwa ya watu, ni ya ustawi wa pamoja kwa wananchi wote, ni maendeleo ya kimali na maendeleo ya utamaduni yanayoenda sambamba, ni kuishi pamoja katika hali ya kupatana kati ya binadamu na mazingira ya asili, na ni mambo ya kisasa ya kufuata njia ya maendeleo ya amani.
Chaguo jipya
Msukumo wa China wa maendeleo ya mambo ya kisasa umeanza kuangaziwa huku mabadiliko makubwa ambayo hayajaonekana katika karne hii yakibadilisha Dunia, ambao kwa mara nyingine umefikia njia panda katika historia.
Ingawa maendeleo ya mambo ya kisasa ya nchi za Magharibi yametengeneza utajiri wa nyenzo ambao haujawahi kutokea, njia yake ya umwamba, ukoloni na upanuzi wa mipaka haifai. Njia hii pia imesababisha matatizo ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa pengo la utajiri, upotevu wa rasilimali na uharibifu wa mazingira.
Chama cha CPC kina nia ya wazi kwamba kujenga nchi ya kijamaa ya mambo ya kisasa katika sekta zote ni kazi kubwa na ngumu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma