Lugha Nyingine
(Mkutano Mkuu wa CPC) China yashikilia kithabiti kupanua kufungua mlango kwa pande zote
Zhao Chenxin, Naibu Mkurugenzi wa Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya Taifa akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari katika Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC ambao unaendeleo hivi sasa hapa Beijing, China Oktoba 17, 2022. (Xinhua/Zhang Yuwei)
Naibu Mkurugenzi wa Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya Taifa ya China Zhao Chenxin Jumatatu ya wiki hii alisema, China itashikilia kithabiti kupanua ufunguaji wa mlango kwa pande zote, kuhimiza utandawazi wa uchumi wa dunia uendelee kwa mwelekeo wa uwazi zaidi, shirikishi zaidi, uwiano zaidi na kupata maendeleo kwa pamoja.
Zhao alisema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari wa Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha CPC unaoendelea hivi sasa. Alisema, kuna uelewa usio sahihi kuhusu muundo mpya wa maendeleo chini ya nguzo kuu ya mzunguko mkubwa wa kiuchumi ndani, na wa kuhimizana kwa mzunguko wa kiuchumi wa China na wa kimataifa.
Alisema, maoni kuhusu “ kuchukulia mzunguko mkubwa wa kiuchumi ndani kuwa nguzo kuu” kutapunguza nguvu ya kufungua mlango, hata kuifanya China ielekee kuendeleza “uchumi wa kutegemea uzalishaji wa wenyewe na kujitosheleza” ni maoni yasiyo sahihi.
Alisema, utandawazi wa uchumi wa dunia umekuwa mwelekeo usiobadilika, China imejiunga kwa kina na uchumi wa dunia na mfumo wa kimataifa, China inahusiana na kutegemeana kwa kiwango cha juu na viwanda vya nchi nyingi duniani.
Alisema, kuendeleza hali mpya ya maendeleo kuna umuhimu mkubwa kwa ajili ya China kutimiza maendeleo ya sifa bora zaidi, yenye ufanisi zaidi, ya usawa zaidi, ya endelevu zaidi na salama zaidi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma