Lugha Nyingine
Tanzania kusambaza miche milioni 3 ya mibuni kuhimiza uzalishaji
Bodi ya kahawa ya Tanzania (TCB) imetangaza kuwa itasambaza bure miche milioni 3 ya mibuni aina ya robusta ili kuhimiza uzalishaji wa kahawa nchini Tanzania.
Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa TCB Bw. Priscus Kimaro amesema maandalizi yote yamefanyika na kwamba mibuni hiyo itasambazwa katika mkoa wa Kagera.
Kahawa inalimwa katika mikoa 17 ya Tanzania, na katika miaka ya nyuma uzalishaji ulikuwa ni tani elfu 50 kwa mwaka. Kutokana na juhudi za serikali katika mwaka wa mavuno wa 2020/2021 uzalishaji ulifikia tani elfu 73.
Mkoa wa Kagera unaongoza kwa uzalishaji wa Kahawa aina ya Robusta ukichukua kati ya asilimia 30 na 40 ya nchi nzima, huku mikoa ya Songwe na Ruvuma ikiongoza kwenye uzalishaji wa kahawa aina ya Arabica na kuchukua asilimia 44 ya kahawa aina hiyo nchini Tanzania.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma