Lugha Nyingine
CPC kuendelea kutimiza bila kuyumba lengo la Muungano wa Taifa la China
(Picha inatoka Shirika la Habari la China Xinhua.)
BEIJING – Xi Jinping amesema Jumapili hii kwamba Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kitatekeleza sera yake ya jumla ya kutatua suala la Taiwan katika zama mpya, na kuendelea kutimiza kithabiti lengo la Muungano wa Taifa la China.
"Kutatua suala la Taiwan ni suala la Wachina, jambo ambalo lazima litatuliwe na Wachina," Xi amesema kwenye ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC).
"Tutaendelea kujitahidi kutimiza lengo la muungano wa taifa kwa amani, kwa uaminifu mkubwa na juhudi kubwa, lakini hatutaahidi kuacha kutumia nguvu na tunabaki na chaguo la kuchukua hatua zote muhimu. Hii inalenga nguvu ya nje inayoingilia mambo ya Taiwan na watu wachache wanaotaka kuifanya ‘Taiwan ijitenge', na shughuli zao za ufarakanishaji hailengi ndugu zetu wa Taiwani," amesema.
Xi amesema magurudumu ya historia yanaendelea kuelekea kutimiza lengo la Muungano wa Taifa la China na ustawishaji mkubwa wa Taifa la China. "Lengo la Muungano Kamili wa Taifa la China lazima litimizwe na bila shaka litaweza kutimiza!"
"Siku zote tunaheshimu, kufuatilia na kujitahidi kuleta manufaa kwa ndugu zetu wa Taiwan. Tutaendelea kuhimiza mabadilishano ya kiuchumi na kiutamaduni na ushirikiano katika Mlango wa Bahari wa Taiwan," Xi amesema.
"Tutawahimiza watu wa pande zote mbili za Mlango wa Bahari kushirikiana pamoja ili kuenzi utamaduni wa Taifa la China na kujenga uhusiano wa karibu na maelewano," amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma