Lugha Nyingine
Thamani ya Biashara ya huduma ya China iliongezeka kwa asilimia 20.4 katika miezi minane ya kwanza
Takwimu zilizotolewa na Wizara ya Biashara ya China Jumatano iliyopita zilionyesha kuwa thamani ya biashara ya huduma ya China katika miezi minane ya kwanza ya mwaka 2022 iliongezeka kwa asilimia 20.4 ikilinganishwa na ile ya kipindi kama hicho mwaka uliopita.
Kwa mujibu wa takwimu, thamani ya jumla ya biashara ilifikia Yuan trilioni 3.94 (sawa na dola za Marekani milioni 554.13 hivi). Na thamani ya huduma ya biashara nje ya nchi ilifikia Yuan trilioni 1.91, na iliongezeka kwa asilimia 23.1 kuliko ile ya kipindi kama hicho mwaka uliopita, na thamani ya huduma ya biashara ya uagizaji bidhaa ilifikia Yuan trilioni 2.03, na imeongezeka kwa asilimia 17.9 ikilinganishwa na ile ya kipindi kama hicho mwaka uliopita.
Huduma za shughuli za utalii zilirejea katika hali ya kuongezeka kipindi hiki, thamani yake iliongezeka kwa asilimia 7.1 kuliko ile ya kipindi kama hicho mwaka uliopita na kufikia Yuan bilioni 542.66.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma