Lugha Nyingine
Mauzo ya Mwezi Septemba ya magari ya Jianghuai ya China yaongezeka kwa asilimia 13.82
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 13, 2022
Aprili 21, Mwaka 2022,mfanyakazi akifanya kazi kwenye mstari wa kuunda malori katika kituo cha uzalishaji cha Kampuni ya Kundi la Magari ya Jianghuai, katika Mji wa Hefei, Mkoa wa Anhui, China. (Mpiga picha:Bai Bin/Xinhua) |
Kampuni ya Kundi la Magari ya Jianghuai ya Anhui ilitoa takwimu zikionesha kuwa, thamani ya mauzo ya jumla ya mwezi Septemba limeongezeka kwa asilimia 31.9 ikilinganishwa na ile ya kipindi kama hicho mwaka uliopita.
Kampuni hiyo iliuza magari 47,700 mwezi uliopita, na mauzo ya miezi tisa ya kwanza ya mwaka 2022 yamefikia magari 371,700 kwa jumla.
Kutoka Mwezi Januari hadi Mwezi Septemba, kampuni hiyo pia iliuza magari 79,800 kwa nchi za nje, hili ni ongezeko la asilimia 31.9 kuliko lile la kipindi kama hicho mwaka uliopita.
Takwimu za Shirikisho la Viwanda vya Magari la China zinaonesha mauzo ya magari ya China yameongezeka kwa asilimia 25.7 mwezi Septemba kuliko yale ya kipindi kama hicho mwaka uliopita.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma