Lugha Nyingine
IMF yapunguza makadirio ya ukuaji wa uchumi wa dunia kwa mwaka ujao kuwa asilimia 2.7
Mwanauchumi mkuu wa IMF Pierre-Olivier Gourinchas (pili kushoto) akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Washington, D.C., Marekani, Oktoba 11, 2022. (Picha/Xinhua)
Ripoti mpya kuhusu makadirio ya uchumi wa dunia iliyotolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inakadiria kuwa, ukuaji wa uchumi duniani utaongezeka kwa asilimia 3.2 mwaka huu, kiasi ambacho kinalingana na makadirio yaliyowekwa mwezi Julai, na ukuaji huo utaendelea kupungua na kufikia hadi asilimia 2.7 mwaka ujao, kiasi ambacho kiko chini ya makadirio yaliyowekwa mwezi Julai.
Ripoti hiyo imeeleza kuwa, hivi sasa uchumi wa dunia unakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo kiwango cha juu cha mfumuko wa bei za bidhaa, mazingira mabaya ya fedha, mgogoro wa Ukraine na kuendelea kwa maambukizi ya korona.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma