Lugha Nyingine
Marais wa China na Ujerumani watumiana salamu za pongezi kwa kuadhimisha miaka 50 tangu nchi hizo kuanzisha uhusiano wa kibalozi
Rais Xi Jinping wa China na Rais Frank-Walter Steinmeier wa Ujerumani wametumiana salamu za pongezi katika maadhimisho ya miaka 50 tangu nchi hizo mbili kuanzisha uhusiano wa kibalozi.
Katika salamu zake, Rais Xi amesisitiza kuwa, katika miaka 50 iliyopita, kwa kufuata moyo wa kuheshimiana na kunufaishana, China na Ujerumani zimeendelea kuboresha uhusiano wao, na kutoa mchango kwa amani na maendeleo duniani. Amesema anatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Ujerumani, na yuko tayari kushirikiana Rais Steinmeier kuchukulia maadhimisho hayo ya miaka 50 kama fursa ya kuendeleza zaidi uhusiano wa wenzi wa kimkakati kwa pande zote kati ya nchi hizo mbili.
Naye Rais Steinmeier amesema, katika miaka 50 iliyopita, uhusiano kati ya Ujerumani na China umepata maendeleo makubwa katika sekta mbalimbali, jambo ambalo limeimarisha mawasiliano ya nchi hizo na ustawi wa watu wao. Ameongeza kuwa China ni mwenzi mkubwa zaidi wa kibiashara wa Ujerumani, na ushirikiano wa uchumi na biashara unafuata maslahi ya nchi hizo mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma