Lugha Nyingine
Ongezeko la Mapato ya Wachina Laenda Sambamba na Upanuzi wa Uchumi
Wateja wakinunua vitu kwenye kituo cha maduka huko Guangzhou, Mkoa wa Guangdong wa Kusini mwa China. (Xinhua/Huang Guobao)
Idara ya Takwimu ya kitaifa ya China Jumanne ya wiki hii ilisema, katika mwongo uliopita mapato ya wakazi wa China kimisingi yanaenda sambamba na upanuzi wa uchumi wa nchi, na pengo kati ya mapato ya wakazi wa mijini na wa vijijini limepungua kwa kiasi fulani.
Mnamo mwaka 2021, wastani wa mapato ya kila mtu yanayoweza kutumika yalifikia Yuan 35,128 (sawa na Dola za Marekani 4,940), ambao umeongezeka kwa asilimia 112.8 kuliko mwaka 2012. Idara hiyo ya takwimu ilisema, baada ya kuzingatia bei za bidhaa zilizopanda, wastani wa ongezeko halisi la mapato hayo ya kila mtu kwa mwaka yalifikia asilimia 6.6, ambayo yanalingana kimsingi na upanuzi wa uchumi.
Katika mwongo uliopita, pengo kati ya mapato ya wakazi wa mijini na vijijini limepungua kwa kiasi fulani.
Wastani wa matapo yanayoweza kutumika ya kila mkazi wa mijini yalifikia Yuan 47,412 mwaka 2021, ambao umeongezeka kwa asilimia 96.5 kuliko mwaka 2012. Wastani wa mapato yanayoweza kutumika ya kila mkazi wa vijijini yalifikia Yuan 18,932, ambao umeongezeka kwa asilimia 125.7 ukilinganishwa na mwaka 2012.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma