Lugha Nyingine
Rais wa Kenya adhamiria kupunguza ukopaji unaofanywa na serikali
Rais William Ruto wa Kenya ameahidi kuwa atadhibiti ukopaji wa ndani na nje unaofanywa na serikali ili kuchochea ongezeko la uchumi.
Rais Ruto ambaye amefungua bunge la 13 la Kenya, amesema ukopaji mkubwa wa serikali umedunisha mchango wa sekta ya biashara kwenye fedha za serikali na uwekezaji. Amesema katika kipindi cha miaka mitatu ijayo, serikali itafanya juhudi ili kuhakikisha kwamba fedha za matumizi ya serikali zinakuwa chini ya mapato yanayokusanywa na serikali.
Amesema kwa sasa bajeti ya Kenya ina nakisi ya dola bilioni 7.45 zinazotakiwa kukopwa, na pia ameiagiza hazina kufanya kazi na wizara kuhakikisha wanaokoa dola za kimarekani bilioni 2.48.
Rais Ruto pia amesema Mamlaka ya Mapato ya Kenya (KRA) inakusanya dola bilioni 19.04 kwa mwaka, ambazo hutumiwa kulipa mishahara ya watumishi wa umma na kuhudumia madeni.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma