Lugha Nyingine
Viongozi wa China na Japan watumiana salamu za kupongeza miaka 50 tangu nchi hizo zianzishe uhusiano wa kibalozi
Rais Xi Jinping wa China na waziri mkuu wa Japan Kishida Fumio wametumiana salamu za pongezi kufuatia miaka 50 tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi.
Kwenye salamu zake, rais Xi amesema katika miaka 50 iliyopita, kutokana na juhudi za pamoja za serikali na watu, China na Japan zimefikia maoni mengi ya pamoja na kuzidisha mawasiliano na ushirikiano katika sekta mbalimbali, na kuleta manufaa muhimu kwa nchi hizo mbili na wananchi wao, na pia kuhimiza amani na utulivu wa kikanda na kimataifa.
Fumio amesema Japan inapenda kushirikiana na China kuanzisha uhusiano tulivu wa kiujenzi, na kuhimiza amani na ustawi wa nchi hizo mbili, wa kikanda na wa kimataifa.
Waziri mkuu wa China Li Keqiang na Fumio pia wametumiana salamu za pongezi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma