Lugha Nyingine
Marais wa China na Argentina watuma barua za pongezi kwa jukwaa la mawasiliano ya kiutamaduni kati ya nchi hizo mbili
Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Argentina Alberto ángel Fernández wametuma barua za pongezi kwa nyakati tofauti kwa Jukwaa la ngazi ya juu la mawasiliano ya kiutamaduni kati ya nchi hizo mbili.
Kwenye barua yake rais Xi amesema China na Argentina ni marafiki wakubwa na washirika wazuri, na huu ni mwaka wa 50 tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi, na pia ni mwaka wa ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili. Anatumai kuwa washiriki wa jukwaa hilo watachangia busara na kukusanya maoni ya pamoja ili kuandika ukurasa mpya kwenye uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Argentina, na kutoa mchango katika kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya.
Kwa upande wake, rais Fernández wa Argentina amesema kwenye barua yake ya pongezi kuwa ushirikiano wenye ufanisi kati ya vyombo vya habari vya Argentina na China umezidisha maelewano kati ya watu wa nchi hizo mbili, na anatarajia kuwa pande hizo mbili zitaimarisha ushirikiano ili kutoa mchango zaidi katika kukuza maslahi ya watu wa nchi hizo mbili na maendeleo ya amani ya dunia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma